LIGI kuu ya Zanzibar juzi ilifikia tamati kwa mchezo uliowakutanisha mabingwa wa ligi hiyo KMKM na Mlandege ambao ulimalizika kwa mabingwa hao kushinda bao 1-0.

Mchezo huo ambao uliambatana na ugawaji wa zawadi kwa bingwa huyo ulichezwa kwenye uwanja wa Amaan na kushuhudiwa na mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud.