WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohamed, amewataka madiwani kusimamia ukusanyaji wa mapato ndani ya mabaraza yao ya miji.

Alisema, madiwani ni sehemu ya viongozi wa mabaraza ya miji wenye wajibu kama wakurugenzi, hivyo wanatakiwa kusimama imara kuhakikisha mapato ya serikali yanakusanywa.