MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania iliyokutana hapa Zanzibar, imesikiliza kesi 32 kati ya kesi 33 zilizopangiwa kusikilizwa katika mahakama, hiyo huku mashauri 28 yamepatiwa uamuzi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kesi kwa mahakama ya wazi zilizoendeshwa katika mahakama kuu ya Zanzibar, mwenyekiti wa mahakama hiyo Shaaban Ali Lila alisema kikao cha mahakama hiyo kilianza Mei 30 na kumalizika rasmi Juni 17 mwezi huu.