MTENDAJI mkuu wa Manchester United Richard Arnold alifanya mazungumzo nje ya nyumba yake ya Cheshire kwa kukutana na baadhi ya mashabiki katika baa yake ya mtaani.
Sehemu ya mjadala huo ilirekodiwa kwa siri na kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii.
Pia anasema pesa ambazo meneja mpya Erik ten Hag na mkurugenzi wa soka John Murtough wanataka kutumia kwa wachezaji wapya “zipo”.
Inafahamika kuwa mazungumzo yanaendelea na Barcelona kuhusu kiungo Mholanzi Frenkie de Jong, ambaye ndiye anayelengwa na Ten Hag kwenye usajili wa majira ya kiangazi.
United hawajashinda Ligi kuu tangu 2013 na mara ya mwisho walishinda kombe mwaka 2017. Walimaliza msimu uliopita katika nafasi ya sita, baada ya kumfukuza Ole Gunnar Solskjaer na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa muda Ralf Rangnick.
Arnold alielezea msimu uliopita kama “jinamizi” lakini pia alikosoa maandamano ya mashabiki ambayo yalifanyika kwenye mechi nyingi za mwisho za klabu za nyumbani za msimu huu.
Mashabiki walifanya maandamano mbalimbali kupinga umiliki wa familia ya Glazer wa klabu hiyo ya Old Trafford msimu uliopita katika michezo ya nyumbani na uwanja wa mazoezi.
Mnamo Mei 2021, maandamano ya mashabiki yalisababisha mchezo wao wa nyumbani wa ligi kuu dhidi ya Liverpool kuahirishwa.
Mnamo Januari 2020, nyumba ya makamu mwenyekiti mtendaji Ed Woodward ya Cheshire ilishambuliwa na mashabiki.
Arnold alikua Mkurugenzi Mtendaji tarehe 1 Februari 2022, kufuatia kuondoka kwa Woodward.