MASHABIKI wa Simba wamemuaga kiungo mshambuliaji Rally Bwalya na kumtunza pesa baada ya mechi dhidi ya KMC
ambapo hiyo ilikuwa mechi yake mwisho akiwa na kikosi cha Simba.
Tukio hilo limetokea baada ya mechi hiyo kumalizika kwa ushindi wa mabao 3-1, ambapo Bwalya alizunguka uwanja mzima kuaga mashabiki akiwapungia mikono kama ishara ya kuwaaga huku wao wakimtunza pesa kuonyesha mapenzi yao.