MAWAZIRI wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wameeleza kwamba katika kipindi kifupi kijacho mji wa Zanzibar utakuwa na mabadiliko makubwa yenye kwenda sambamba na maendeleo ya kiuchumi.

Kauli hiyo waliitoa wakati wakichangia bajeti kuu ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka wa fedha 2022/2023 na kujibu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Chukwani.