HOSPITALI Kuu ya Mnazimmoja imenunua vitanda maalum 50 kwa ajili ya wagonjwa wanaokatika mifupa kutokana na ajali vyenye thamani ya shilingi milioni 160.

Akizungumza na Zanzibar  Leo ofisini kwake hivi karibuni, Mkurugenzi huduma za waauguzi, Muhidini Ussi Haji, alisema vitanda hivyo vitatumika katika wodi za mifupa za wanawake, wanaumme na watoto.