NAIBU Waziri wa Afya, Hassan Khamis Hafidh, amewataka wauguzi wanaoshughulikia miradi mbalimbali kurudi katika vituo vya afya, ili kuendelea  kutoa huduma kwa  wananchi.

Hayo amesema katika ziara ya kuangalia utendaji kazi kwa vituo vya afya vinavyotoa huduma ya mama na mtoto katika kituo cha afya Mpendae na Sebleni Wilaya ya Mjini, amesema kurudi kwa wauguzi hao itasaidia kuondoa usumbufu uliopo katika vituo hivyo.