NEW DELHI, INDIA

TAASISI ya haki za binadamu ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vitendo vya kibaguzi dhidi ya Waislamu nchini India.

Taasisi hiyo imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuiwajibisha India kwa ukiukaji wa haki za binadamu za walio wachache na kukomesha uhasama wao.

Tume Huru ya Kudumu ya Haki za Kibinadamu (IPHRC), mojawapo ya vyombo vikuu vya OIC yenye wanachama 57, iliandika kwenye Twitter kwamba inalaani vitendo hivi  vya kikatili vya ubaguzi, vinavyokiuka maadili yote ya jamii anuai na ambavyo vinafanyika kwa kupuuza sheria .

IPHRC imetoa wito kwa jamii ya kimataifa na hasa taasisi husika za Umoja wa Mataifa kuitaka serikali ya India kulinda haki za binadamu za Waislamu waliowachache nchini humo na kusitisha mara moja uhasama dhidi yao.

Aidha asasi hiyo ya OIC imezitaka taasisi  za Umoja wa Mataifa ziihimize serikali ya India iheshimu haki za binadamu za  Waislamu walio wachache na kukomesha mara moja uhasama dhidi yao.

Tume hiyo pia imesambaza klipu ya Arundhati Roy, mwanaharakati na mwandishi maarufu wa India, akielezea jinsi India ilivyogeuka kuwa biashara Kihindu .

Kauli ya IPHRC kuhusu dhuluma dhidi ya Waislamu nchini India inakuja baada ya tume hiyo kuidhinisha taarifa za OIC na  jamii ya kimataifa za kulaani na matamshi machafu yaliyotolewa na viongozi wa chama tawala India, BJP, dhidi ya Mtume Mtukufu Muhammad (SAW).

Juzi pia Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa alitoa indhari kuhusu kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia.

Halikadhalika wiki iliyopita  Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) ulitoa mwito wa kupasishwa sheria ya kujinaisha na kupiga marufuku kuvunjiwa heshima matukufu ya dini mbalimbali kote duniani.