NCHI zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani zimeamua kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka duniani.

Zimekubaliana kuongeza uzalishaji kwa mapipa 648,000 kwa siku mwezi ujao.

Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano uliofanyika kwa njia ya video wa mawaziri wa Umoja wa Nchi zinazozalisha Mafuta kwa wingi Duniani na washirika wake ikiwemo Urusi.

Kundi hilo linalojulikana kama OPEC+ linasema nchi wanachama zitaongeza uwezo wa uzalishaji ili kukidhi kiwango kipya.

Kiasi hicho ni takribani mapipa 200,000 kwa siku ikiwa ni ongezeko la uzalishaji linalozidi lile lililokuwa limepangwa awali.