KAMPALA, UGANDA
WIZARA ya Afya imeazimia kuharibu shehena ya dozi 150,000 za chanjo ya Sinopharm Covid-19 iliyotolewa kwa Uganda mwezi Machi na serikali ya Mauritius kupitia Wizara ya Mambo ya nje.
Uamuzi huo wa Wizara ya Afya ulifuatia barua ya Aprili 13 ya Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kitaifa ya Dawa (NDA), Dk Medard Bitekyerezo kwa Waziri wa Afya, Dk Jane Ruth Aceng, iliyosema kuwa walikagua shehena hiyo na kubaini haifai kutumika kwa sababu ya ukiukwaji wa sheria katika uagizaji na uhifadhi.
Kuharibu chanjo hizo zinazouzwa kwa bei ya dola 30 (Sh 113,000) kwa dozi, inamaanisha kuwa nchi itaharibu dozi zenye thamani ya Sh17b.
Dk Bitekyerezo alieleza katika barua hiyo kwamba shehena ya chanjo ya Sinopharm, iliyowasili Machi 1, bila wao kujua, ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la Kenya, haikuwa na kumbukumbu za joto.
Data ya halijoto ni muhimu ili kufuatilia ufuasi wa viwango vya joto vya uhifadhi, ambayo ni sehemu muhimu ya kuhakikisha uwezo wa chanjo unadumishwa.
Dkt Aceng alikuwa ameamuru NDA kukagua shehena hiyo kufuatia ombi kutoka kwa waziri wa Mambo ya Nje, Jenerali Jeje Odongo, kuhusu shehena hiyo, kulingana na vyanzo.
Emmanuel Ainebyoona, msemaji wa wizara ya Afya, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu bado hajaiona barua hiyo.
Dk Aceng alipendekeza kwamba kwa sababu ya mambo haya, chanjo, ambazo bado ziko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe, ziharibiwe.
Jenerali Odongo hakuweza kupatikana ili kutoa maoni yake kuhusu hatua ya Wizara ya Afya kuharibu misimamo hiyo.
Lakini Waziri wa Mashauri ya Kigeni, Henry Oryem Okello, alisema Wao ni wataalamu, ni uwanja wao wa utaalam kujua kama kitu ni kizuri au kibaya.
Haya yanajiri wakati serikali inatatizika kumaliza takriban dozi milioni 44.7 za chanjo ilizopata kwa kiasi kikubwa kupitia michango na nyengine kupitia ununuzi wa moja kwa moja.
Takriban Waganda milioni 16 wamechanjwa kwa dozi moja, huku zaidi ya milioni 10.9 wakiwa wamechanjwa kikamilifu tangu zoezi hilo lianze Machi 2021, kulingana na wizara hiyo.
Lengo la awali lilikuwa ni kutoa chanjo kwa takriban watu milioni 22, ambao wana umri wa miaka 18 na zaidi lakini hii imeongezwa hadi kwa wale walio na umri wa miaka 12 au zaidi katika hatua ya kudhibiti janga hili na kuhakikisha ufufuo wa uchumi.