Gianluca Scamacca
KLABU ya Paris Saint-Germain imekubaliana masharti na Skriniar pamoja na kiungo wa kati wa Lille na Ureno, Renato Sanchez (24) na mshambuliaji wa Italia, Gianluca Scamacca (23) ambaye anaichezea Sassuolo. Mabingwa hao wa Ufaransa sasa watalazimika kuweka makubaliano na klabu hizo tatu. (Get French Football News).
Lisandro Martinez
KLABU ya Arsenal imewasilisha ofa ya pauni milioni 35 kwa mlinzi wa Ajax, Lisandro Martinez na wanaonekana kuiongoza Manchester United katika kinyang’anyiro cha kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24. (Mirror).
Raphina
CHELSEA inakaribia kuafikiana na Leeds kuhusu dau la kumnunua mshambuliaji wa Brazil, Raphina (25) , ambaye pia anazivutia klabu kama vile Arsenal na Barcelona (Guardian).
Milan Skriniar
CHELSEA imebadilisha mawazo yake na sasa inamnyatia beki wa Milan na Slovakia mwenye umri wa miaka 27, Milan Skriniar ambaye pia analengwa na PSG baada ya kubaini kwamba kifungu cha kumuuza mchezaji wa Juventus na Uholanzi, Matthijs de Ligt (22), ni ghali mno. (Mail)
Oleksandr Zinchenko
CHELSEA inahusishwa na harakati za kumnunua mchezaji mwengine wa tatu wa Manchester City. ‘The Blues’ inataka kumnunua mshambuliaji wa Ukraine, Oleksandr Zinchenko (25), baada ya kuanzisha mazungumzo ya kutaka kumsaini mshambuliaji wa England, Raheem Sterling (27), na pia kuhusishwa na usajili wa beki wa Uholanzi, Nathan Ake (27). (Mail).
Frenkie de Jong
MENEJA wa Manchester United, Erik ten Hag, anatumai kumsaini kiungo wa Uholanzi, Frenkie de Jong (25), kutamshawishi kiungo mchezeshaji wa Denmark, Christian Eriksen (30), kujiunga na klabu hiyo ya Old Trafford. (Star).
Richarlison
KLABU ya Tottenham wameimarisha harakati zao za kutaka kumsaini mshambuliaji wa Everton na Brazil, Richarlison (25) lakini, ombi la pauni milioni 20 ambalo lilishirikisha winga wa Uholanzi, Steven Bergwijn (24), limekataliwa na ‘The Toffees’. (Telegraph).
Djed Spence
KLABU ya Middlesbrough imakasirishwa na hatua ya Tottenham kusitisha makubaliano ya kumnunua beki wa kulia wa England chini ya umri wa miaka 21, Djed Spence na hilo linaweza kufungua milango ya Nottingham Forest kumnunua mchezaji huyo mwenye umri miaka 21 ambaye aliisaidia City kupanda hadhi ya kucheza Ligi Kuu England msimu uliopita. (Football League World).
Cheick Doucoure
KLABU ya Crystal Palace inakaribia kumsaini kiungo wa Lens, Cheick Doucoure katika makubaliano yenye thamani ya euro milioni 21 pamoja na marupurupu kwa mchezaji huyo wa Mali mwenye umri wa miaka 21. (Guardian).
Andreas Pereira
KLABU ya Fulham imeruhusiwa kuzungumza na kiungo wa kati wa Brazil, Andreas Pereira baada ya kukubaliana na Manchester United, ijapokuwa mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 26 anataka kusalia Flamengo ya Brazil ambapo yupo kwa mkopo. (90 Min).
Josh Brownhill
KLABU ya Southampton imeunga na klabu nyegine baada ya kuvutiwa na kiungo wa Burnley na England, Josh Brownhill. (90 Min).
Sam Edozie
KLABU ya Manchester City imekubali kumuuza mchezaji wa England anayechezea timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19, Sam Edozie (19), kwa klabu ya Ujerumani Bayer Leverkusen kwa dau la pauni milioni 10. (Football Insider).