WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Masoud Ali Mohammed, amesema serikali iko katika hatua za mwisho za kuvunja mkataba na kampuni zilizopewa kandarasi za ujenzi wa masoko.

Waziri huyo alieleza hayo wakati alipofanya mazungumzo na mwandishi wa habari hizi, ambapo alisema itavunja mikataba ya ujenzi wa masoko, kwani hauonekani ufanisi kwenye ujenzi.