Kila mmoja wetu anaelewa kuwa ili nchi ikamilike iwe na vikosi vya kijeshi, vikosi ambavyo vinahitaji kuwa na vifaa vya kutosha, kutengewa bajeti kila wakati, na kuimarishwa pamoja na kusimamiwa kama vikosi vya jeshi chini ya serikali.

Kwa kawaida jeshi linaundwa kwa lengo la kujihusisha na vita na kulinda nchi dhidi ya maadui wa ndani na nje, lakini wakati mwingine linashiriki katika shughuli za kutoa msaada kama vile kusambaza chakula, maji na matibabu wakati nchi inapohitaji.

Jeshi linalozungumziwa hapa ni kama jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) au ni kama majeshi ya Rwanda na kadhalika.

Lakini zipo nchi nyingi huru ambazo bado zinakataa kuunda vikosi vya kijeshi.

Hivyo, Makala hii itazungumzia baaadhi ya taifa ambayo hayana jeshi kubwa kama ilivyozoweleka kwa nchi mbali mbali hapa ulimwenguni.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Shirika la kimataifa la kijajusi la Marekani, CIA, kuna makumi ya nchi ulimwenguni ambazo hazioneshi uwepo wa kijeshi.

Inaelezwa kuwa, kwa mfano, nchi ya Uswisi na Austria zilikubali kuilinda Liechtenstein, huku Ufaransa na Hispania ziliilinda Andorra.

Hata hivyo, CIA iliongeza kuwa ingawa nchi hizi “hazina jeshi la kudumu”, nchi kadhaa zina jeshi la polisi, ambalo linaweza kufanya kazi kama jeshi la kulinda nchi na mipaka yake.

Katika oroda hiyo nchi mashuhuri zisizo na jeshi ulimwenguni ni pamoja na:

MAURITIUS

Inaelezwa kuwa, Mauritius ilivunja jeshi lake mwaka 1968, lakini ina Kikosi Maalumu kidogo, kilichofunzwa vyema.  Ambao wanashirikiana vyema katika masuala ya usalama nan chi ya India.

Mauritius ni mojawapo ya nchi chache duniani ambazo hazina jeshi la kudumu la kulinda nchi.

Hata hivyo, nchi hiyo ina maafisa wa polisi wapatao 10,000, ambao wana jukumu la kutekeleza kila kitu ambacho wanajeshi, polisi na vikosi vya usalama vingefanya. Mauritius ni kivutio maarufu cha watalii barani Afrika.

ANDORA

Andorra ni nchi ndogo ya milima iliyopo katikati ya Ufaransa na Hispania. Nchi hiyo haina jeshi la kudumu, hata hivyo, ina makubaliano ya ulinzi na nchi za Hispania na Ufaransa.

Na bado ina askari wa kujitolea wasio na silaha, ambao huonekana kwenye sherehe maalum. Sheria za nchi zinatekelezwa na polisi wa kitaifa, ambao wanahusika na usalama wa nchi.

COSTA RICA

Costa Rica ilivunja vikosi vyake vya kijeshi mnamo 1948, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kila mwaka tarehe mosi Desemba, nchi hiyo huadhimisha siku ya kuvunjwa jeshi.

Hata hivyo, nchi hiyo ina kikosi cha polisi kilichopewa mafunzo maalum na Marekani na Colombia, ambacho kinahusika na usalama wa ndani.

Nchi hiyo ya Amerika ya Kati iko karibu na ikweta na ina pwani zinazounganisha Bahari ya Carrebean na Bahari ya Pasifiki.

LIECHTENSTEIN

Nchi hiyo ilivunja jeshi lake mnamo 1868, ikiona kuwa na jeshi ni gharama kubwa.

Liechtenstein ina kikosi cha polisi kilicho na silaha ndogo ndogo, ambacho kinafanya shughuli za usalama wa ndani.

Aidha inapokea usaidizi wa ulinzi kutoka Uswizi na Austria ikiwa wanahitaji usaidizi, kulingana na makubaliano yasiyo rasmi yaliyoafikiwa na nchi hizo tatu.

PANAMA

Jeshi la Panama lilivunjwa mwaka 1990 na sasa lina kikosi kidogo kilichofunzwa kijeshi, na nchi hii ina kile kinachoitwa Jeshi la Wananchi wa Panama, ambalo linahusika na usalama wa ndani na matatizo ya mpaka.

ICELAND

 

Iceland ilikuwa na jeshi mnamo 1869, lakini tangu wakati huo nchi hiyo imeingia makubaliano na Marekani, ambayo kutoka 1951 hadi 2006 imekuwa ikisaidia Vikosi vya Ulinzi vya Iceland.

Mwaka 2006, Marekani ilitangaza kutoa msaada wa kiusalama kwa Iceland, kwa kuwa haikuwa na jeshi nchini humo.

Usalama wa nchi hii ni wajibu wa Muungano wa NATO (hasa Marekani, Norway, na Denmark).

Aidha sio nchi hizo tu ambazo hazina jeshi la kudumu, kwamujibu wa CIA kuna maeneo mengi sana ambayo yameorodheshwa kuwa hayana jeshi la kudumu duniani, miongoni mwa ni :

Aruba Cayman Islands Cook Islands Curacao Falkland Islands Faroe Islands French Polynesia Greenland Grenada Kiribati.

Marshall Islands Federated States of Micronesia Monaco Montserrat New Caledonia Nauru Niue Palau St. Lucia St. Vincent and the Grenadines Samoa San Marino Sint Maarten Solomon Islands Svalbard Tuvalu and Vanuatu.