MELFU ya watu wamelazimika kuikimbia moto katika nchi mbali mbali ikiwemo Ufaransa,Ureno, na Uhispania pia hali hiyo imeibuka katika eneo la Alaska, kaskazini mwa Arctic , na katika maeneo yote ya kaskazini  mwa Canada.

Aidha imeshuhudiwa kuwa sio muda mrefu tangu moshi kuonekana ukitanda katika maeneo yaliyoungua ya misitu ya Argentina mchana  na katika mji mkuu wa Paraguay.  Moto katika maeneo hayo na mengine ambayo hayajaorordheshwa imekuwa ni changamoto kubwa, lakini suala la kujiuliza ni je, mataifa yana vifaa vya kutosha kuweza kukabiliana matukio hayo ya mara kwa mara?

Wataalamu wanasema kwamba”moto usiyo wa kawaida unaotokana na mabadiliko ya hali ya hewa isiyo ya kawaida”,

Kutokana na mabadiliko hayo ya hali ya hewa yanayosababisha ukosefu wa mvua na upepo mkavu zinasababisha kuibuka kwa moto katika misitu hiyo, na kupelekea vyanzo vya moto mara kwa mara takriban ya maeneo yote ya dunia.

Wachambuzi wanasema kuwa, mabadiliko ya hali ya tabia nchi yanaifanya mimea kuwa rahisi zaidi kuungua na udongo kuwa mkavu zaidi, na mara kwa mara hali hii inapotokea huwa ya muda mrefu na, kubwa na mbaya zaidi.

Lakini athari hutofautiana kwa kila kanda na nyingine na inaweza kusababishwa na mambo mengine.

Mwandishi wa makala ya hivi karibuni ya tathmini katika fizikia ya jiografia anasema baadhi ya maeneo yenye misitu katitudo ya juu yalishuhudia ongezeko la 50% au zaidi la eneo linaloungua katika miongo miwili ya kwanza ya karne.

Hatahivyo, katika maeneo ya joto ya Afrika idadi za moto wa kwenye misitu ilipungua katika kipindi hicho hicho, kutokana namabadiliko ya matumizi ya ardhi, ikiwa ni pamoja na kupanuka kwa ukulima. Na hili, wataalamu wanasema inapunguza kwa ujumla idadi ya moto wa misituni kote duniani, pamoja na eneo linaloungua kwa ujumla.

“Maeneo ya Savana nayabakia kuwa yenye kutawanyika na ndio maana yanashuhudia moto michache,” anasema Dkt. Niels Andela, mwanasayansi anachunguza maeneo ya mbali yanayoweza kukabiliwa na moto katika taasisi ya  BeZero Carbon. “Na kwasababu yanachukua hadi 70% ya moto ya dunia, tunashuhudia kupungua kwa jumla ya matukio ya moto wa msituni kwa dunia nzima.”

Huku kukiwa na ongezeko la ziada la joto, tatizo la moto wa msituni linatarajiwa kuwa baya zaidi katika maeneo mengine.

Kwamujibu wa ripoti ya mpango wa mazingira wa Umoja wa Mataifa iliyochpishwa mapema mwaka huu ilitabiri ongezeko la ‘’moto mkubwa’’ kwa dunia hadi 14% ifikapo mwaka 2030, na 50% kufikia mwisho wa karne.

Ilikuwa tu baada ya kufikia moto walipogundua ni kwa kiwango gani ni mkubwa,”   mwanakijiji, Ghulam Sakhi. “Upepo ulikuwa mkali sana na ilikuwa inasamabaza miali ya moto.”

Binamu zake Sakhi, Kalaa Khan, 35, na Mohammad Noor, 30, walijikuta wakizuiwa kuona kutokana na moshi mkubwa. Kwa kukanganyikiwa walijipata wakitembea kuelekea usawa wa moto, na wakashinda kuudhibiti, anasema mjane ambaye lazima sasa alazimike kujaribu kuishi bila mume wa kumsaidia kuitunza familia.

“Hatuna usaidizi, hatuna raslimali za kupambana na mioto ya aina hiyo ya nyikani,” anasema Sakhi,

Maafisa wa udhibiti wa maafa hawakufahamu kuhusu moto, anasema mwanaharakati wa mabadiliko ya hali ya hewa Salmeen Khpalwak, na mwanzoni hakujibu ombi la usaidizi.

Siku kadhaa baadaye helikopta ilitumwa kumwaga maji kwenye moto, bila mafanikio.

Ilikuwa tu pale Iran ilipotuma ndege yenye uwezo wa kumwaga maelfu ya maji ndipo sehemu kubwa ya moto ilipozima. Kwa hatua hii takriban 40% ya hekari 26,000 ya msitu imeangamia, vyanzo vya eneo hilo viliiambia BBC.

Zaheer Mirza, ambaye anafanya kazi katika mbuga ya wanyama ya Margalla Hills karibu na mji mkuu wa Pakistani, Islamabad, anasema wafanyakazi pale pia wana ukosefu wa ujuzi na vifaa vya kuzima moto.

Kuuzima moto, kwa kiasi kikubwa hutegemea vizima moto vya kujitengenezea nyumbani, asnasema. Kuzuia mioto kusambaa hutengeneza breki za mioto, ” lakini vifaa hivi vimeonyesha kuwa havifai na mioto inaendela kuwa mibaya zaidi “.

Katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi mara nyingi huwa linazungumziwa suala la uwepo wa fedha zilizotumiwa kuzuia kupunguza kiwango cha hewa ya kaboni na gesi nyingine zinazoongeza joto angani na ni machache sana yaliyotekelezwa, au kusaidia nchi kufanya mabadiliko yanayoweza kuzisaidia kukabiliana na athari za tabia nchi.

Aidha kuhusu pesa zilizotumiwa katika utekelezaji, ni chache zilizoelekezwa katika kusaidia kukabiliana na mioto ya msituni, anasema Duncan Macqueen wa taasisi ya kimataifa ya mazingra na maendeleo.

Wakati alipokuwa akifanya kazi mjini Belize miaka michache iliyopita, Macqueen alifahamu kwamba kulikuwa na mradi mmoja tu wa mafunzo ya moto ya msituni, yaliyodhaminiwa na Huduma za misitu za Marekani.

Hivyo kutokana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza ambapo kwa aslilimia kubwa waachambuzi wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, basi jumuiya za kimataifa zinazohusiana na majanga mbali mbali zinapaswa kufanya juhudi za makusudi kwa ajiki ya kutoa vifaa na mafunzo ya kupambana na janga hilo la kimaumbile.