Skip to content

rawhiya

Dk. Mwinyi anogesha furaha Zanzibar Heroes 

NA KHAMISUU ABDALLAH  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajia kuunda kamati maalum ya kumshauri namba bora ya kukuza soka la Zanzibar.  Dk. Mwinyi alieleza hayo katika hafla ya chalula cha mchana aliyoiandaa kwa ajili yakuwapongeza mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup timu ya Taifa ya Zanzibar,… Read More »Dk. Mwinyi anogesha furaha Zanzibar Heroes 

Dk. Mwinyi: Mazoezi kinga madhubuti ya maradhi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyiamewataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kufanya mazoezi kwani ni kinga madhubutidhidi ya maradhi hasa yasioambukiza. Dk. Mwinyi aliyasema hayo katika viwanja vya Mnazimmoja Wete wakati akizungumza nawananchi waliojikeza katika bonanza la mazoezi kitaifa lililoambata na na matembeziyaliyoanzia katika uwanja wa mpira Kinyasini hadi uwanja wa Mnazimmoja, Wete Pemba. Alieleza kuwa kufanya mazoezi kutaweza kupunguza na kuondosha maradhi yasioambukizayakiwemo ya kisukari, presha pamoja na unene uliyokithiri. Aidha Dk. Mwinyi alifahamisha kuwa kuwa maradhi yasioambukiza yamekuwa yakiongezekasiku hadi siku yakilinganishwa na maradhi yanayoambukiza ambayo yalikuwa yakiongoza katikamiaka iliyopita. “Niwaombe sana ndugu wananchi, tusiache kufanya mazoezi kwani kufanya mazoezikunapelekea kujikinga na maradhi yasioambukiza,  hili tuelewe wazi”, alieleza Dk. Mwinyi. “Lakini pia niwafahamishe wana michezo wenzangu kuwa mazoezi ni afya, hivyo tuendeleekufanya mazoezi ili tuweze kuweka miili yetu sawa”, alieleza Dk. Mwinyi. Sambamba na hayo Rais Mwinyi aliwataka wananchi wa Zanzibar kuendelea kudumisha hali ya amani, umoja na utulivu uliopo nchini hasa katika kipindi hiki nchi ikielekea katika uchaguzimkuu hapo baadae. “Niwaombe sana viongozi wa dini na wanasiasa kuendelee kuwahubiria wafuasi wetu juu ya umuhimu wa kuitunza amani ya nchi iliyopo”, alisisitiza Dk. Mwinyi.  Mapaema Dk. Mwinyi aliupongeza uongozi wa Chama cha Wafanya Mazoezi Zanzibar (ZABESA) kwa kuwashajihisha wananchi kuendelea kufanya mazoezi pamoja na kuendelezasiku ya mazoezi kitaifa nchini. Aidha… Read More »Dk. Mwinyi: Mazoezi kinga madhubuti ya maradhi

Macron auona upande wa pili wa shilingi barani Afrika

  • Makala

WAKATI Ufaransa ikiendelea kupoteza kambi zake kadhaa za kijeshi barani Afrika, raiswa nchi hiyo, Emmanuel Macron, katika safari ya kimyakimya kwenye kituo cha mwishocha operesheni za nchi hiyo huko Djibouti, amekiri kwamba Afrika inapitia kwenyemabadiliko. Kwa mujibu wa rais huyo sababu kuwepo kwa mabadiko aliyoyashuhidia barani Afrika ni kutokana na maoni ya umma na serikali za nchi hizo na kueleza kuwa nafasi ya Ufaransa banihumo nayo lazima ibadilike. Katika safari hiyo, Macron amekiri kwamba kambi ya kijeshi ya Ufaransa nchini Djibouti inaweza kuwa na nafasi muhimu zaidi na kukiri kuwa Ufaransa inalazimika kubadilishamtazamo wake wa zamani dhidi ya uwepo wa majeshi yake barani Afrika. Macron pia ametangaza kuwa majukumu ya kambi ya kijeshi ya Ufaransa huko Djibouti yataangaliwa upya na kusema kambi hiyo inapaswa kutumika kama sehemu ya utumiaji nguvukatika baadhi ya misheni za Ufaransa barani Afrika.… Read More »Macron auona upande wa pili wa shilingi barani Afrika

Upatu: Mbinu yakujikwamua yenye tamu na chungu

  • Makala

NA MWANDISHI WETU KUCHEZA upatu imekuwa ni mtindo ambao wanawake wengi wamekuwa wakitumiakama njia ya ya kujikwamua kupata fedha au mtaji kwaajili ya kuendesha shughulimbalimbali za maisha yao ya kila siku.  Wanawake saba katika kundi la wanawake 10 waliofanya mahojiano na makala haya wamewahikushiriki katika aina mbalimbali za upatu.  Hata hivyo mtindo huo umekua ni fursa yenye tamu na chungu inayowakabili wanawake wengikutokana na changamoto za mfumo wa uendeshaji wake.  Upatu upo aina mbalimbali kulingana na mfumo wa uendeshaji wake, kwa mfano upatu wa hisaambao ambao kundi la wanawake wanaungana katika kuweka kiasi kidogo kupata fursa ya kukopa kiwango maalumu bila riba ya marejesho. Pia kuna aina ya upatu unaohusisha vikundi vya ushirika, upatu wa vikundi vidogo vya uwekajina ukopaji kwa riba ambao maarufu mitaani kama (kausha damu), na nyengine.  Upatu unafanyika katika maeneo ya kazi mfano maofisini, majirani, na hata kwa wanafamilia.  Mtindo uliozoelekea zaidi upatu ni wa vikundi vidogo vya wasichana na wanawake katika maeneo ya makazi ambao wanaungana na kuweka utaratibu wa kuchangiana kiwango maalumucha pesa ambacho kila mshiriki atalamizika kutachangia kila baada ya muda.  Vikundi hivi ambavyo mara nyingi inakuwa ni majirani, marafiki au familia vinakuwa na kiongozi maalumu anaechaguliwa miongoni mwa wanakikundi maarufu kama “kijumbe”.… Read More »Upatu: Mbinu yakujikwamua yenye tamu na chungu