LUANDA, ANGOLA MAZUNGUMZO yaliyopangwa kufanyika ya kuwakutanisha rais wa Rwanda na Jamhuriya Kidemokrasia ya Congo DRC nchini Angola, kwa ajili ya kumaliza mgogoro wa mashariki mwa DRC, yamefutwa. Maofisa wamesema kuwa, kulikuwa na matarajio makubwa kwamba, marais wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wangelikutana juzi kwa mualiko wa Rais wa Angola. Hata hivyo, mazungumzo hayo yamefutwa. Mkuu wa ofisi ya Rais wa Angola aliwaambiawaandishi wa habari kwamba kinyume na matarajio, mkutano umeshindwa kufanyika. Kwa upande wake ofisi ya rais wa DRC imesema kuwa, mazungumzo hayo hayakufanyikakutokana… Read More »Mazungumzo baina ya Kagame, Tshisekedi yavunjika