Skip to content

Kitaifa

Waziri Haroun aeleza mkakati wa  kuimarisha mawasiliano, uchumi

  • Zanzibar

NA MWANAJUMA MMANGA WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawathamini wananchi wake ndio maana inaendelea kujenga barabara za kisasa ili kurahisisha mwasiliano na kuimarisha uchumi wao.   Waziri Haroun aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kidimni –Ubago, wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unmguja, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar. Alisema kufunguliwa kwa barabaraba hiyo kwa matumizi ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo kwani kutatanua wigo  na kuimarisha uchumi wa watu wa maeneohayo wakiwemo wakulima, wafanyabiashara na kinamama pale wanaokwendakujifungua. “Bila shaka wananchi wa maeneo hayo wanajivunia na matunda ya mapinduzikwani kwao ni faraja hivyo ni vyema kuhakikisha tunaendeleza kutunzamiundombinu hiiili itusaidia kwa usafiri wa watu na mazao yanapoyatoamashambani. “Serikali ya awamu ya nane inayopongozwa na Rais wa Zanzibar… Read More »Waziri Haroun aeleza mkakati wa  kuimarisha mawasiliano, uchumi

Miundombinu ya kisasa  itaharakisha  upatinajaji haki – Dk. Shein

  • Zanzibar

RAIS mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya saba, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuimarishamiundombinu ya kisasa inayohakikisha wananchi wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria. Ameeleza hatua hizo ni pamoja na kujenga majengo ya kutosha ili kesi   zinazowasilishwa mahakamani zipate nafasi ya kuendeshwa na kutolewa mamuzikwa haraka zaidi  ili kupunguza mrundikano. Dk. Shein alieleza hayo wakati wa ufunguzi wa jengo la mahakama ya mkoa wa Kaskazini Unguja huko pale na kuongeza kuwa hapo awali mahakama ilikuwa na majengo finyu yaliyosababisha kuchelewa kutolewa kwa maamuzi hivyokuchelewesha upatikanaji wa haki kwa wananchi. Aidha rais huyo mstaafu alieleza kuwa inapendeza kuona sasa kuna majengomazuri na yenye nafasi pamoja na vitendea kazi watu jambo litakalochochea kasiya upatikanaji wa haki kwa wakati. “Huu ni ushahidi kwamba Zanzibar ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria inayojengwa kwa kuwepo mihimili mitatu ya serikali, Baraza la Wakilishi na Mahakama  ambayo ni misingi muhimu duniani katika utekelezaji wa utawalabora”, alieleza Dk. Shein. Aidha Dk, shein aliwataka wananchi kutumia mahakama kutoa ushahidi pale wanapohitajika ili kusaidia kupatika kwa haki kwani ushahidi ndio unaopelekeamtu kupata haki hivyo wananchi wasihofie. Vile vile aliwataka Majaji na Mahakimu kufuata sheria na kutoa haki kwa wananchi kwani jambo la haki limetajwa hata nadani ya vitabu vitukufu vya dini hivyo wanapaswa kuwa waadilifu. Naye Mtendaji Mkuu wa mahakama, Kai Bashir Mbarouk, akisoma ripoti  ya kitaalamu juu ya ujenzi huo , alisema… Read More »Miundombinu ya kisasa  itaharakisha  upatinajaji haki – Dk. Shein

Dk. Mwinyi: Tutajenga uwanja mfano wa  ‘Old Traford’

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujenga uwanja mkubwawa michezo wenye hadhi ya kimataifa, kitakachotumika kwa michuano ya kimataifaikiwemo michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027. Dk. Mwinyi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na wadau wa michezo waliohudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa viwanja vya michezoMaisara (Maisara Sports Complex), mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar. “Tuna dhamira ya kweli ya kujenga uwanja wa kisasa wa… Read More »Dk. Mwinyi: Tutajenga uwanja mfano wa  ‘Old Traford’

TANESCORuvuma kufikisha huduma ya umeme kila kitongoji

  • Bara

NA STEPHANO MANGO, SONGEA SHIRIKA la Umeme Tanzania, TANESCO, mkoa waRuvuma, limesema litahakikisha kila mwananchi wa mjinina vijijini anafikiwa na huduma ya umeme  ili kuongezamatumizi ya nishati safi ya kupikia. Akizungumza na wakazi wa mkoa wa Ruvuma, Zachariah Julius Stephano kutoka TANESCO, aliwahimiza wananchikujijengea utaratibu wa kutumia nishati safi ya kupikia kwagharama nafuu na salama. Alisema watu wasihofu kutumia nishati safi ya kupikiakama vile majiko ya umeme na vifaa vyote vya mapishivinavyotumia umeme. Badala yake alisema watumie kwa wingi kwani vifaa vyotevimetengenezwa kutumia kiwango kidogo cha umemeambapo uniti moja ya umeme mteja anaweza kupikachakula cha familia. Kwa upande wake, Mhandisi wa mita za luku, Brown Mkole, aliwataka wateja wa TANESCO kuwa na utaratibuwa kufanya ukarabati wa miundombinu ya nyaya zaumeme kila baada ya miaka 10 ili kujihakikishia usalama. Alisema kama mteja anapata changamoto ya matumizi yaumeme kuwa juu tofauti na kiwango anachodhaniametumia, ajitahidi kutoa taarifa ili kuwasaidiwa.

INEC yasisitiza uwazi daftari la wapiga kura

  • Bara

NA MWANDISHI WETU TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema uwepowa mawakala kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kurani kielelezo cha uwazi kwenye zoezi la uboreshaji wadaftari la kudumu la wapiga kura. Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya watendajiwa daftari ngazi ya mkoa mkoani Mbeya, Mwenyekiti waINEC, Jaji Jacobs Mwambegele, alisema pamoja nakuhakikisha zoezi linafanyika kwa uwazi mawakala haopia watasaidia kuwatambua wananchi wanaoombakuandikishwa. “Wakati wa uboreshaji wa daftari mawakala wa vyama vyasiasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikishawapiga kura. Jambo hili ni muhimu kwani litasaidia kuletauwazi katika zoezi zima lakini pia mawakala haowatasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyokupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima,” alisema.  Aliongeza kuwa mawakala hao hawaruhusiwi kuwaingiliawatendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yaovituoni. Akizungumza wakati wa kufungua mkutano kama huomkoani Iringa, Makamu Mwenyekiti wa INEC, Jaji(Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk, alisema katikakuhakikisha zoezi hilo linakuwa la uwazi, Tume imetoakibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshajiwa daftari kwa asasi za kiraia 157 na asasi za kiraia 33 kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hilo. “Ni muhimu kutoa ushirikiano kwa asasi hizo zitakapofikakwenye maeneo yenu kwa ajili ya kutekeleza majukumuyao. Tume itawapa vitambulisho kwa urahisi wakuwatambua,” alisema Jaji Mbarouk.  Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi yauboreshaji wa daftari mkoani mbeya, iringa na mkoa wadodoma kwenye halmashauri ya wilaya ya mpwapwaambapo uboreshaji utafanyika kwa siku saba kuanziaDisemba 27 Januari 02, 2025.

WEMA, ZICTIA zasaini mkataba kuunganisha skuli 100 Mkongo wa Taifa 

  • Zanzibar

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali, imetiliana saini hati za mashirikiano na Shirika la Mawasiliano la Zanzibar (ZICTIA) kwa ajili ya kuweka Mkonga wa mawasiliano kwa skuli 100 za Unguja na Pemba. Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu, Waziri… Read More »WEMA, ZICTIA zasaini mkataba kuunganisha skuli 100 Mkongo wa Taifa