Skip to content

Fadlu ajivunia Kamara,Manula

NA TIMA SALEHE,DAR ES SALAAM

KOCHA mkuu wa klabu ya Simba,David Fadlu amejivunia walinda mlango wale Aish Manula na Moussa Kamara kuwepo katika timu za Taifa ya Tanzania na Guinea.

Wachezaji hao wawili ambao wanagombea namba kwenye lango la klabu ya Simba chini ya kocha Fadlu juzi walikuwa wanazipambania timu zao za taifa kwenye mchezo wakuwania kufuzu kucheza AFCON 2025 nchini Morocco.

Mchezo huo ulichezwa kwenye Dimba la Benjamini Mkapa,Jijini Dar es Salaam na Taifa Stars dhidi ya Guinea ambao ulimalizika kwa Taifa Stars kushinda 1-0 huku Guinea

Katika lango Stars alisimama Aishi Manula ambae kwasasa kwenye klabu ya Simba anakosa namba langoni akisimama Moussa Kamara ambaye juzi alisimama kwenye lango la Guinea.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii kocha Fadlu aliandika kwamba nifahari kuona makipa wake wawili wanapata nafasi ya kuanza kwenye timu zao za taifa.

Kocha huyo alihitimisha kauli hiyo kwa kuandika kuwa hao ndio Simba wawili wa klabu yake.