RIO DE JANEIRO, Brazil
KLABU ya Cruzeiro imefikia makubaliano ya uhamisho wa winga, Arthur Gomes kwenda Dynamo Moscow, imesema, miamba hiyo ya ‘Serie A’ ya Brazil.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atakuwa na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Urusi hadi Juni 2029 katika mkataba unaoripotiwa kuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 7.5 pamoja na nyongeza.
“Cruzeiro inathibitisha uhamisho wa kudumu wa Arthur Gomes kwenda Dynamo Moscow,” klabu hiyo ya Belo Horizonte ilisema katika chapisho la mtandao wa kijamii. “Tunamshukuru mshambuliaji huyo kwa taaluma yake na kujitolea kwa Cruzeiro na tunamtakia mafanikio mengi katika kazi yake.”
Gomes alifunga mabao manane na kutoa pasi tano za mabao katika mechi 59 alizocheza kwenye michuano yote akiwa na Cruzeiro kufuatia uhamisho wake wa 2023 kutoka Sporting Lisbon.
Anakuwa Mbrazil wa pili kwenye kikosi cha Dynamo Moscow, akiuungana na kiungo Bitello. (Goal).