Skip to content

GUARDIOLA AELEZA MAN.UNITED ILIVYOMPA MATESO

LONDON, England

PEP GUARDIOLA anasema usingizi wake uliteseka baada ya kichapo cha kushangaza kutoka kwa Manchseter United.

Guardiola alionekana mwenye furaha baada ya City kuongoza  kupitia kwa Josko Gvardiol dakika ya 36.

Dakika 88 Matheus Nunes alimpa Amad Diallo mpira kabla ya kuongeza makosa yake kwa kumfanyia madhambi mshambuliaji huyo alipokuwa akijaribu kurekebisha makosa yake. Bruno Fernandes alifunga bao kwa mkwaju wa penalti.

Dakika mbili baadaye wakati mpira mrefu wa Lisandro Martinez uliomkuta Diallo kutoka pembeni na kumwacha Guardiola na wachezaji wake wakishangaa.

City ambao sasa wamepoteza mechi nne kati ya 105 za nyumbani za ligi kuu chini ya Guardiola ambapo wamekuwa mbele hadi mapumziko, wakishinda 94 na sare saba.

Guardiola aliiambia Match of the Day: “Sina uwezo wa kutosha. Mimi ndiye bosi. Mimi ndiye meneja. Ni lazima nitafute suluhu na hadi sasa sijapata. Huo ndio ukweli.

“Sina mengi zaidi ya kusema. Hakuna ulinzi. Manchester United walikuwa wavumilivu. Hatujapoteza mechi nane katika misimu miwili. Hatuwezi kujilinda.

Guardiola alipendekeza kwamba marekebisho makubwa yatasubiri hadi msimu wa joto.

Matarajio yao ya Ligi ya Mabingwa pia yako hatarini baada ya kupoteza tena, wakati huu dhidi ya Juventus huko Turin.

Guardiola ana kila sababu ya kutaja majeruhi, hasa kwa Rodri na pia John Stones pamoja na wengine, lakini hii haiwezi kutumika kisingizio cha kushuka kwa viwango hivyo.