MWENYEKITI wa Huduma za Jamii ya Baraza la Jiji la Zanzibar, Abdullatif Omar Haji, amesema hatua za dharura zinahitaji kuchukuliwa mara moja kutokana na kuzuka kwa maradhi yanayodhaniwa kuwa ni kipindupindu kwa kushirikiana na taasisi zote za serikali zinazohusika na masuala ya huduma za jamii zikiwemo manispaa na vitengo vya Wizara ya Afya.
Abdulllatif aliyasema hayo alipokutana na watendaji wanaosimamia Kamati za huduma za jamii katika Manispaa ya Mjini, Manispaa Magharibi ‘A’ na Magharibi ‘B’ katika ofisi za Baraza la Jiji zilizomo katika jengo la Michenzani Mall, mjini Zanzibar.
Aidha alisema hali maradhi iliyopo sasa hairidhishi hata kidogo na taasisi hizi zisipokua makini katika kutekeleza majukumu yako basi hali hiyo inaweza ikawa ya hatari zaidi.
Hata hivyo alisema ipo haja kwa kila mmoja wao kuchukua juhudi za makusudi ili kuhakikisha majaa yasiyo rasmi na yaliyo rasmi kuondoshwa mara moja ili kuweza kuinusuru hali iliyopo isizagae zaidi.
Aidha Abdullatif aliwataka watemdaji hao wa huduma za jamii kutoka manispaa zote kupita katika maeneo yote ya biashara kutoa elimu juu ya kuzihifadhi buashara zao na kuwaeleza hali halisi iliyo ili kudhibiti mripuko huu usiendeleee.
Akizungumzia masuala ya mtambuka, Abdulllatif alisema ipo haja pia kuanza kutoa elimu kwa jamii kupitiq midahalo vyombo vya habari kuhusiana naasuala ya udhaliliishaji, mazingira na maradhi ya Ukimwi ili jamii izidi kupata uelewa kwa vile jamii inaonekana imejisahau sana kwa kushamiri kwa vitendo hivyo siki hadi siku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha wa Baraza la Jiji, Rahma Ali Khamis, alisema ipo haja ya kuanzishwa kwa oparesheni maalumu zikazosimamiwa viongozi wakuu wa manispaa ili kuona sasa suala hili linachukuliwa kitaifa.
Aidha alishauri kuweka bajeti maalum ya kununu vifaaa vya kufanyia usafi katika majaa na mitaro ikiwemo gari za taka na za ufatiliaji kwa vile hivi sasa manispaa zote zina uhab wa vitendea kazi.
Kwa upande wao watendeji hao walisema ukosefu wa bajeti ya mafuta za kuondesha paeresheni zao ndizo zinazo dhoretesha ufanyaji wa kazi zao kwa vile Mafuta huyo la kila baada ya miezi mitatu ili kukabili hatari zinazoweza kujitokeza.