MWANZONI mwa mwezi Mei mwaka huu, eneo la pwani ya Afrika Mashariki kilikaribia kupigwa kwa kimbunga kilichopewa jina la HIDAYA.
Kwa mujibu wa wataalamu kimbunga hicho ambacho kilionesha kila dalili ya kusababisha uharibifu mkubwa kilififia na kupoteza nguvu kilipofika katika kisiwa cha Mafia.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania ilieleza kuwa kimbunga hicho kilipiga kisiwa cha Mafia saa tatu asubuhi mnamo Mei 4, takriban kilomita kilomita 130 kusini mashariki mwa mji wa kibiashara nchini Tanzania Dar es Salaam kabla ya kupoteza nguvu zake.
Hata hivyo pamoja na kufifi na kupoteza nguvu kimbunga HIDAYA, kimesababisha maafa katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashari ikiwemo mvua na upepo mkubwa ulioshuhudiwa.
Kumbukumbu zinabainisha kuwa kwa mara ya mwisho kimbunga kilipiga mnamo mwaka 1952 wakati huo ikiwa Tanganyika na kilitua mkoani Lindi katika pwani ya kusini ya Tanzania.
Ama kwa upande mwengine kimbunga kwa mara ya mwisho kilipiga visiwa vya Zanzibar nmano mwaka 1872, ambapo athari za kimbunga hicho zilifika mpaka upande wa bara katika eneo la Bagamoyo, kaskazini mwa Dar es Salaam.
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikilengwa sana kupigwa na vimbunga ambapo vimbunga viwili vilivyokaribia kuipiga nchi hiyo ni Kenneth cha mwaka 2019.
Aidha mnamo mwaka 2021 Tanzania pia ilikuwa kwenye hatari kubwa ya kupigwa na kumbunga Job, lakini hata hivyo kilipunguza makali na hakikusababisha maafa yeyote makubwa.
HIDAYA kilikuwa kimbunga cha tatu kwa miaka ya hivi karibuni kutishia kupiga Tanzania, hata hivyo wakati sehemu mbalimbali duniani ambazo zipo katika ukanda wa pwani huathirika na vimbunga, baadhi ya watu wanaweza kujiuliza kwa nini Tanzania na upwa wa Afrika Mashariki (Kenya na Somalia) haziathiriwi na vimbunga?
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya masuala ya hali ya hewa, kimbunga cha mwisho kuipiga Tanzania ikiwa miaka 80 imepita lakini vimbunga vyengine vilivyotabiriwa kuipiga Tanznaia vilififia.
Kimbunga kilichopiga Zanzibar Zanzibar, kwa mujibu wa maelezo yaliyorekodiwa ya balozi wa Uingereza visiwani Zanzibar wa miaka hiyo John Kirk theluthi mbili ya mashamba ya minazi na karafuu visiwani humo yaliharibiwa vibaya.
Hivyo, laiti Jobo kingetua na nguvu, basi kingekuwa kimbunga cha kwanza kurekodiwa kupiga jiji la Dar es Salaam na cha pili kuipiga Zanzibar baada ya takriban miaka 149.
Eneo la bahari ya hindi, kuanzia kusini magharibi ya India mpaka upwa wa mashariki na kusini ya Afrika una msimu wake wa vimbunga ambao huanza mwezi wa Novemba na kuishia mwezi wa Aprili.
Vimbunga vya Zanzibar na Lindi vyote vilitokea mwezi wa nne, hata kwa upande wa Jobo pia huu ni mwezi wa Aprili.
Kimbunga Kenneth kilipiga mwezi wa Aprili 2019 na mwezi mmoja nyuma yake kimbunga kibaya zaidi cha Idai kiliipiga Msumbiji na athari zake kufika mpaka nchi jirani za Malawi na Zimbabwe.
Kwa msimu wa mwaka 2020/21 ambao unaelekea mwisho zaidi ya vimbunga vikubwa na hafifu 16 vimejitengeneza na kuathiri baadhi ya nchi katika ukanda huo, Jobo ikiwa ni kimoja wapo.
Suali liliopo ni kwa nini vimbunga hivyo havianzii ama kuathiri pwani ya Afrika Mashariki? Jibu ni kuwa eneo hilo lipo katikati ya dunia.
Dunia imegawanyika katika mihimili miwili, mhimili wa kusini na mhimili wa kaskazini. Kilichogawanyisha dunia katika mihimili hiyo ni mstari wa kufikirika unaoitwa Ikweta. Mstari huo unapita kwenye nchi 13 duniani zikiwemo Somalia, Kenya na Uganda.
Profesa Marshall Shepherd, rais wa zamani wa Jumuiya ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Marekani, alisema vimbunga husukumwa na nguvu iitwayo Kani ya Coriolis.
Alisema kani hiyo haina nguvu kabisa katika eneo la Ikweta kwa kuwa ndipo mhimili wa Kaskazini na Kusini hupakana
Profesa Marshall Shepherd, alisema kuwa hali ya upepo katika mihimili hiyo huenda katika njia tofauti upande mmoja kushoto upande mwengine kulia,”
Mtaalamu huyo alieleza katika makala yake ya mwaka 2018 iliyochapishwa na jarida la Forbes kuwa nguvu hiyo kinzani ndio huua nguvu ya vimbunga katika eneo hilo la Afrika Mashariki.
Japo Tanzania haijapitiwa na mstari wa Ikweta lakini ipo katika ukanda wa Ikweta, masafa machache kusini mwa mstari huo uliopita katika nchi jirani za Kenya, Uganda na hata DR Congo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Prof Shepherd endapo kimbunga kikali kitajitengeneza mbali na eneo hilo kinaweza kuathiri moja kwa moja eneo hilo, japo kutokea kwa hali hiyo ingali bado ni jambo la nadra.
Hata hivyo, hali ya mvua kubwa na mafuriko huukumba ukanda wa Ikweta kutokana na athari ya vimbunga vinavyopiga maeneo ya karibu katika eneo hilo.