LONDON, England
LIVERPOOL na Newcastle wapo mbioni kumenyana katika kinyang’anyiro cha kuwania moja ya mali moto zaidi kwenye Ligi Kuu ya England, Bryan Mbeumo.
Vinara wa sasa wa ligi, liverpool na wababe hao wa Geordie wote wanamfuatilia Mbeumo ambaye kiwango chake akiwa Brentford msimu huu kimekuwa cha kusisimua.
Kocha, Eddie Howe kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa na mshambuliaji huyo, ambaye amefunga mabao manane katika mechi 11 za Ligi Kuu ya England zilizoanza msimu huu.
Lakini, mshambuliaji huyo wa Cameroun sasa amevutia umakini kwa Arne Slot.
Anamchukulia mshambuliaji huyo wa Brentford kama chaguo bora kwa Liverpool kutokana na uwezo wake wa kubadilika.
Liverpool wamekuwa wakimsaka mshambuliaji huyo msimu mzima na sasa wanafikiria kumnunua mchezaji huyo majira ya kiangazi.
Anaonekana hata kama mbadala wa Mo Salah ambaye hatma yake ndani ya Liverpool bado haijafahamika.
Skauti kutoka St. James Park pia wamekuwa wakimtazama mchezaji huyo, ambaye Howe anaaminika kumchukulia kama shabaha yake kuu.(Goal).