MSTAHIKI Meya wa Jiji la Zanzibar, Mahmoud Muhamed Mussa, ameitaka kampuni ya GIZ inayofanya kazi ya upembuzi yakinifu ajili ya uchakataji maji taka katika mitaa ya Zanzibar kuharakisha zoezi hilo ili waikabidhi kampuni itakayofanya kazi hiyo muda ukifika.
Mahmoud alieleza hayo alipokuwa akifungua mkutano wa uwasilishwaji kwa ripoti ya awaali ya upembezi yakinifu kwa wadau mbali mbali wa taasisi za serikali ikiwemo Wizara ya Maji na Manispaa za Unguja pamoja na Madiwani wa Baraza la Jiji la Zanzibar katika ukumbini wa mikutabo wa baraza hilo Michenzani Mall, Zanzibar.
Aliiambia kampuni hiyo kuwa muda ulipo si rafiki hivyo ipo haja kukamilisha hatua hiyo ya awali ili waendelee na hatua ya pili mapema Januari 2025 na kuhakikisha mambo yaliyobakia yanamalizika Kwa vile wananchi wamekua na shauku ya kuona mradi huo unaanza mara moja ili waondokane na kadhia wanazopitia hivi sasa.
Alisema Baraza la Jiji limejipanga kuleta mabadiliko makubwa katika utekelezaji wa mradi huo huku wakitaka kwenda na kasi ya maendeleo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.
“Tunawaomba ripoti ya mwisho ipatakane Disemba 23, mwaka huu ili ifakapo mwakani kila kitu kiwe kimeshakaa katika eneo lake kwa ajili ya utekekelezaji”, alieleza Meya huyo.
Kwa upande wao kampuni GIZ walisema wamejipanga vyema katika kuhakikisha ripoti ya ya awali wanaikamilisha kwa wakati ili waanze upembuzi yakinifu wa awamu ya pili haraka iwezekanavyo.
Kwa upande Mshauri Elekezi wa mradi huo, kampuni ya GKW walisema wanahakikisha wanasimamia ipasavyo ili kuona mradi huo unaleta tija kubwa kwa wananchi wote wa Maeneo husika na wanzanzibar kwa ujumla.
Mradi wa uchakataji taka umelenga kufanyika katika maeneo mbali mbali ya Unguja ili kuona Zanzibar inaondokana na kadhia ya maji machafu kwa kuhifadhiwa vyema na kutumika kwa masuala mengine ya kibinaadamu.