NA VICTORIA GODFREY
NCHI tano zimethibitisha kushiriki mashindano ya mpira wa kikapu ya klabu bingwa kwa wanawake Kanda ya Tano ya kufuzu Mabingwa wa Afrika.
Mashindano ya kufuzu yamepangwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 27 hadi Novemba 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa ndani wa Amaan Zanzibar.
Akizungumza na Zanzibarleo kamishna wa mipango na maendeleo wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF) Aloyce Renatus,alitaja nchi za Kenya,Uganda ,Rwanda na wenyeji Tanzania.
Alisema wanatarajia Ethiopia na Sudan Kusini watathibitisha ushiriki wa klabu zao hapo baadae.
” Mwaka huu sisi Tanzania ni wenyeji wa mashindano hayo na tunatarajia zaidi ya klabu 12 zitashiriki ,” alisema Renatus.
Kamishana huyo alisema maandalizi yanaendelea na tayari kamati imeundwa na wajumbe kutoka Tanzania bara na visiwani na watakaa kikao wiki hii kufanya tathmini.