NA SAIDA ISSA, DODOMA
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imezidua gari lenye thamani ya zaidi shilingi milioni 300 huku wakitoa rai kwa jamii kuacha kujichukulia sheria Mkononi.
Akizungumza Mara baada ya uzinduzi wa gari hilo Katika Ofisi za Tume jijini Dodoma Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora Mathew Mwaimu amesema kumekuwepo na matukio mengi ya watu kujichukulia sheria mkononi jambo ambalo sio zuri.
“Tunazungimzia Tanzania nchi inayopaswa kufuata utawala wa sheria hivyo kwa lolote linalotokea mtu ni wazi kila mmoja anapaswa kuhakikisha kwamba anapona jambo la hatari anapaswa kutoa taarifa katika vyombo stahili na vyombo hivyo vitaweza kuchukua hatua zinazostahili,”alisema Jaji Mwaimu.
Alisema sio jambo jema kuondoa uhai wa mtu bila kufuata utaratibu wa kisheria.
Aidha akizungumzia gari hilo alisema uzinduzi wa basi hilo litawasaidia namna ya kuwafikisha watumishi wa Tume katika maeneo yao ya kazi na kupunguza gharama za usafiri.
“Gari hili linakwenda kusaidia katika utendaji kazi hasa pale tutakapokuwa tunasafiri mikoani kwasababu moja ya shughuli za Tume nikutoka nje ya ofisi kwaajili ya kufanya uchunguzi, kutoa elimu kwa umma, na kwenda kufanya tafiti hivyo gari hili linakwenda kusaidia kazi nyingine nyingi zinazotekelezwa na Tume,”alisema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi alisema basi hilo limenunuliwa kwa fedha za ndani kwamaana ya serikali imetoa pesa ili linunuliwe basi kwaajili ya kutoa huduma kwa watumishi wa tume.
“Tume hii ni moja wapo ya tume muhimu Sana ya ndani ya serikali yetu ambayo inasimamia Haki za binadamu,”alisema.
Aidha alieleza katika kuwawezesha kufanyakazi vizuri serikali ikaona kuna umuhimu wa tume kuwa na chombo chake cha usafiri kitakachowasaidia watumishi wake katika utumishi wake wa umma.
“Umuhimu wa tume hii ambayo inatuangalia Sisi kama watanzania na shughuli zetu tunazofanya na inatambulika kimataifa kwaajili ya Haki za binadamu ndani ya nchi,”alisema Katibu Mkuu huyo.