Skip to content

Nyota taifa stars waguswa ajali ya gorofa Kariakoo

NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

MLINDA mlango wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania, Aish Manula, ametoa pole kwa wahanga wa ajali ya ghorofa iliyotokea Kariakoo jijini Dar es Salaam,ajali ya jengo hiyo liliporomoka Novemba 16.

Akizungumza na vyombo vya habari jana, Manula alisema anatoa pole kwa wahanga wote wa ajali hiyo.

Alisema janga hilo ni la kitaifa, ambapo watanzania wapo kwenye majozi makubwa, ambapo ametoa  pole kwa wananchi na taifa kwa jumla juu tukio hilo.

Kwa upande wake nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, alisema anamajozi  kutokana na sakata hilo na anatoa pole.

“Inawezekana huna ndugu au mtu wakaribu katika janga hilo, lakini wote waliopo pale niwatanzania hivyo inaumiza sana, na tunaishukuru serikali kwa juhudi zake katika kuokoa,”alisema.