MOSCOW, URUSI
RAIS wa Urusi Vladimir Putin, ametia saini amri ya kuongeza idadi ya wanajeshi wa Urusi hadi vitengo 2,389,130, wakiwemo wanajeshi milioni 1.5.
Amri mpya, iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi kwa maelezo ya kisheria, itaanza kutumika kuanzia tarehe 1 Disemba 2024.
Hivi sasa, idadi ya vikosi vya jeshi la Urusi ni vitengo 2,209,130, pamoja na wanajeshi milioni 1.32, kulingana na amri ya hapo awali, iliyosainiwa na Putin mnamo Disemba 2023.
Wakati huo huo, wizara ya ulinzi ilisema kwamba vikosi vya jeshi la Urusi vilikomboa makazi ya Uspenovka na Borki katika Mkoa wa Kursk.
Vikosi vya jeshi la Urusi pia vilizuia “mashambulizi matano ya maadui” kutoka pande mbalimbali katika eneo siku hiyo hiyo, wizara iliongeza.