Skip to content

Real Kids yajipanga kuchukua ubingwa

NA ZAINAB ATUPAE

MWENYEKITI wa timu ya Real Kids Nassor Abdalla Zungu,amesema wamejipanga kuchukua ubingwa msimu huu na kuipandisha timu daraja.

Real Kids inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya mjini ambayo imepanda daraja msimu na tayari imechezwa mechi mbili.

Alisema ili kufanikisha malengo yao hayo wameijenga timu katika nafasi zote ili kuona wanakuwa na ushirikiano na kushinda.

“Kupitia uongozi mzima wa timu tunaendelea kuwapa elimu na mazoezi ambayo yataleta mafanikio katika mechi zetu tutakazocheza,”alisema.

Aidha alisema wanachoshukuru kuwa ligi inaendelea vizuri,hivyo waamuzi kuendelea kufanya kazi zao kwa umakini zaidi ili kumaliza ligi salama bila ya migogoro.

Zungu,alisema changamoto inayowasumbua wachezaji ni kucheza mechi zao katika wakati mgumu wa jua kali muda wa saa 7:30 mchana.

“Muda huu sio rafiki kutokana na hali ya hewa ya jua linavyotoa linaumiza,lakini hatuna la kufanya tunaendelea kucheza wachezaji waumia,”alisema.