SANI Abacha alikuwa mmoja kati ya viongozi wa jeshi la Nigeria, ambaye aliongoza mapinduzi na kuchukua madaraka ya taifa hilo kuanzia mnamo mwezi Novemba mwaka 1993.
Abacha alichukua madaraka akiwa kiongozi wa ngazi ya juu katika jeshi la Nigeria wakati huo pia akiwa waziri wa ulinzi wa taifa hilo, ambapo alimuondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Ernest Shonekan.
Hata hivyo, kabla kunyakua madaraka na kuwa rais wa nchi hiyo, Abacha alihusika kikamilifu kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyowaweka madarakani majenarali wa kijeshi kabla ya mwaka 1993.
Wakati alipochukua madaraka, vyombo vya bahari vya nchi za magharibi vilikuwa vikimuelezea kiongozi huyo na kumtaja kama dikteta, kwani serikali yake ilikuwa ikishutumiwa kwenye unyanyasaji na uvinjwaji wa haki za binaadamu.
Katika utawala wake, Abacha anaelezwa alikuwa rais fisadi aliyepora na kuchukua mali za umma kwa maslahi yake binafsi huku fedha alizoiba akizitorosha na kwenda kuficha nje ya nchi.
Kupitia mmoja kati ya washauri wake wa usalama Alhaji Ismaila Gwarzo, alimtumia kufanikisha madili ya ufisadi, ambapo pia mtoto wake aitwae Mohammed naye alihusika kikamilifu kwenye ufisadi.
Katika moja ya ripoti iliyowahi kutolewa nchini humo ilieleza kuwa Abacha na msahauri wake Gwarzo walitengeneza mkataba wa uongo ambao ulitiwa saini na rais huyo, ambapo Gwarzo alikuwa anakwenda kuchukua mamilioni ya fedha benki kuu na kuzipeleka katika nyumba ya Abacha.
Zipo taarifa zinazoeleza kuwa katika utawala wake Abacha alipora kati ya dola bilioni moja hadi dola bilioni tano, utajiri huo unawahusisha wakiwemo baadhi ya wanafamilia yake.
Kilichofuata mwanasheria mkuu alitoa tahadhari kwa benki zote Uswizi akizitaka zitoe maelezo ya akaunti yoyote ile iliyofunguliwa kwa jina la Abacha na washirika wake. “Na ndani ya saa 48, asilimi 95 ya benki zote na taasisi zingine za kifedha zilitangaza walichonacho kile kilichoonekana kwa ajili ya familia.”
Na hatua hiyo ikaweka wazi akaunti zote alizokuwa nazo duniani. “Benki zikatoa maelezo kwa mwendesha mashataka huko Geneva na ningefanya kazi hiyo ya mwendesha mashtaka kwasababu hakuwa na muda wa kuifanya”.
‘Taarifa zilizopatikana kupitia akaunti za benki’. “Tuliona katika kila akaunti pesa hizo zimetoka wapi au pesa hizo zimeenda wapi.
“Maelekezo ya kina juu ya taarifa za malipo ya akaunti hizo pamoja na malipo mengine zilinipa maelezo zaidi ya malipo yaliyofanyika ama kupokelewa au kutolewa kwa nchi zingine.
“Tulikuwa na ushahidi wa aina mbalimbali namna pesa hizo zilivyokuwa zimetumwa maeneo mbalimbali, Bahamas, Nassau, na visiwa vya Cayman – na kwingineko.” Kutafuta mtandao wote aliokuwa nao Abacha ilikuwa kazi kubwa kwa Bwana Monfrini.
“Hakuna aliyeonekana kuelewa kazi hiyo yote ilihitaji juhudi kiasi gani. Nililazimika kulipa watu wengi, mahasibu na mawakili wengi tu kutoka nchi tofauti tofauti.”
“Familia ya Abacha nayo walikuwa wanagombana na kunapigana vita kweli. Walikuwa wanapinga karibu kila kitu. Hatua hii ilichelewesha mchakato mzima.”
Mnamo mwaka 2008, Monfrini aliandika kuwa, kiasi cha dola milioni 508 zilipatikana katika familia ya Abacha kwenye akaunti za benki nchini Uswizi na kurejeshwa kutoka Uswizi hadi Nigeria kati ya mwaka 2005 na 2007.
Kufikia mwaka 2018, kiwango cha pesa ambacho kilikuwa kimerejeshwa Nigeria ni zaidi ya dola bilioni 1.
Wakati alipofariki ghafla bila ya kufaidi mabilioni ya dola aliyoyaiba mamlaka nchini Nigeria ilianza kufanya msako wa kimataifa kujua fedha hizo zimefichwa wapi.
Msako wa fedha hizo umechukua miongo kadhaa ambapo mtu aliyepewa jukumu la kuzitafua fedha hizo alieleza jinsi ambavyo shughuli hiyo ilivyokuwa ikifanyika katika kipindi cha maisha yake.
Mnamo Septemba mwaka 1999, wakili kutoka nchini Uswizi Enrico Monfrini alijibu simu ambayo ilibadilisha maisha yake katika kipindi cha miaka 20 iliyofuata.
“Alinipigia simu usiku wa manane, kama inawezekana nikutane naye katika hoteli aliyokuwepo kwa sababu ya jambo muhimu sana alilotaka kuniarifu. Nikamwambia, ‘Ni usiku lakini sawa tu nitakuja.'”
Sauti ya mtu aliyekuwa akizungumza naye ilisikika kuwa ya ofisa wa juu katika serikali ya Nigeria. ‘Unaweza kutafuta pesa zilizoibwa’?
Monfrini alisema ofisa huyo alipelekwa Geneva na Rais wa Nigeria wakati huo, Olusegun Obasanjo na alitumwa kwenda kutafuta pesa zilizoibwa na Abacha, rais aliyetawala nchi hiyo kuanzia mwaka 1993 hadi kifo chake 1998 kilichotokea ghafla.
Kama wakili, Monfrini alikuwa ameunda mtandao wa raia wa Nigeria aliokuwa na uhusiano mzuri nao tangu miaka ya 1980, waliofanyakazi katika makampuni ya utengenezaji wa kahawa, kakao na bidhaa nyengine.
Alishuku wateja waliokuwa wanapendekezwa na aliyekuwa rais. “Aliniuliza: ‘Unaweza kutafuta pesa hizo na je unaweza kuzizuia? Unaweza kufanya maandalizi pesa hizi zikarejeshwa nchini Nigeria?’
“Nilisema: ‘Ndio.’ Lakini ukweli ni kwamba wakati huo sikujua kazi hiyo inahitaji muda gani kutekelezeka. Na nikalazimika kujifunza kwa haraka sana, kuifanya.”
Ili kuanza kazi hiyo ya uchunguzi, polisi ya Nigeria ilimpatia maelezo kidogo juu ya akaunti za benki za Uswizi za aliyekuwa rais, ambazo zilishukiwa kuwa pesa zilizoibwa na Abacha na washirika wake ziliwekwa kwenye akaunti hizo, Monfrini aliandika katika kitabu alichokipa kichwa ”Kutafuta pesa zilizoibwa”.
Alisema kwamba uchunguzi wa awali uliochapishwa na polisi Novemba 1998, ulibaini kuwa zaidi ya dola milioni 1.5 ziliibwa na Abacha na washirika wake.
‘Madola aliyoiba zilisafirishwa na malori’. Moja ya njia iliyotumika kubeba kiwango kikubwa cha pesa namna hiyo kulihitaji ujasiri.
Abacha alikuwa akimuagiza mshauri wake, amuombee pesa kwa ajili ya suala la usalama na hakuweka wazi pesa hizo zitatumika kwa njia gani.
Baada ya hapo angesaini ombi hilo na mshauri wake kulipeleka Benki Kuu moja kwa moja ambako alitoa pesa hizo, mara nyingi zikiwa ni pesa taslim.
Mshauri wake alikuwa akichukua kiasi kikubwa cha pesa hizo na kuzipeleka nyumbani kwa Abacha. Baadhi ya pesa zilikuwa zikipakiwa kwenye malori zikiwa noti za dola”, alisema Monfrini.
Hii ilikuwa moja ya njia ambayo Abacha na washiriki wake waliitumia kuiba kiasi kikubwa cha pesa.
Njia nyengine zilizotumika zilikuwa ni pamoja na kutoa kandarasi kwa rafiki zake kwa thamani ya juu na kutaka makampuni ya kigeni kulipa kiasi kikubwa cha rushwa ili ziweke kuendesha shughuli zao nchini Nigeria.
Hili liliendelea kwa karibu miaka mitatu hadi kila kitu kilipobadilika pale Abacha alipofariki dunia ghafla akiwa na umri wa miaka 54, mnamo Juni 8, 1998.
Haijafahamika kama alikuwa na ugonjwa wa moyo au alipewa sumu kwasababu mwili wale haukufanyiwa uchunguzi baada ya kufariki dunia, kulingana na aliyekuwa daktari wake alizikwa.
Abacha alifariki dunia kabla ya kutumia mabilioni ya pesa alizoziiba lakini maelezo kidogo tu ya benki yalitumika kama vidokezo kuchunguza pesa hizo zilifichwa wapi.
“Nyaraka zinazoonesha historia ya akaunti zake zilitoa maelekezo kidogo tu ya akaunti zake,” amesema Monfrini. Akiwa na taarifa hizo alipeleka suala hilo kwa mkuu wa sheria nchini Uswizi. Na hapo ndipo alipopata mwanya.
Monfrini alifanikiwa kushawishi familia ya Abacha na washirika wake wa karibu kuanzisha uchunguzi wa kihalifu. Hii ilikuwa ni hatua ya msingi kwasababu ilionesha machaguo mengine ya jinsi mamlaka zinaweza kukabiliana na akaunti zake za benki.