BAGHDAD, IRAQ
IRAQ imezindua sensa ya watu na makaazi nchini kote hapo jana kwa mara ya kwanza baada ya kusimama kwa miaka 27.
Waziri wa Mipango wa Iraq Mohammed Tamim aliwataka Wairaki “kushirikiana na timu za sensa kwa kutoa takwimu sahihi, kwani hii ni muhimu kwa kuunda mustakabali wa Iraqi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo, “Sensa ina umuhimu wa kipekee kwa sababu itachangia katika kuhakikisha haki ya kijamii na kiuchumi na kuboresha kiwango cha huduma katika maeneo yote,” Tamim aliongeza
Mamlaka ya Iraq iliweka vikosi vya usalama katika hali ya tahadhari na kuweka amri ya kutotoka nje wakati wa sensa ya siku mbili katika majimbo yote ya Iraq, ikiwa ni pamoja na yale ya eneo linalotaka kujitawala la Kurdistan.
Iraq kwa kawaida huwa na sensa ya watu kila baada ya miaka 10, na ya mwisho kufanyika mwaka wa 1997. Hakuna sensa iliyofanyika tangu uvamizi wa Marekani wa mwaka 2003.