Skip to content

Tangazo

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar ni Taasisi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoanzishwa kwa mujibu wa Sheria Namba 11 ya ya mwaka 2008. Taasisi hii ina jukumu la kutoa na kusambaza habari, taarifa na sera za serikali kwa umma, kuendesha na kusimamia magazeti ya serikali. 

Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Shirika lina mamlaka ya kuajiri wafanyakazi wapya kwa mujibu wa muongozo uliotolewa na sheria ya Utumishi wa Umma nambari 2 ya mwaka 2011 katika kifungu cha 57(3) na kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2014 katika kifungu nambari 7 (1).

Katika utekelezaji wa Mpango wa Rasilimali watu wa Mwaka 2024/202, Shirika linatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo: –

  1. Mwandishi wa Habari za Kiengereza:  Nafasi 3 Unguja.

Sifa za Muombaji

  • Awe Mzanzibari
  • Asiwe Muajiriwa wa Serikali
  • Awe amemaliza Shahada ya Kwanza au zaidi katika fani ya Uandishi wa Habari (Journalism) au Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha.
  • Awe na umri usiozidi miaka 40.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi za uandishi wa habari za kiengereza katika vyombo vya habari vya kuchapisha (print media) hasa vya Kiingereza, utazingatiwa kama sifa ya ziada.

Majukumu ya Kazi:

  • Kukusanya, kuandika na kuhariri habari na Makala za kiengereza kwa  magazeti ya shirika na kuziweka katika ubora unaohitajika.
  • Kutafsiri habari za kiengereza kwa lugha ya kiswahili na za kiswahili kwa lugha ya kiengereza kabla ya kuchapishwa.
  • Kupanga na kusanifu kurasa za magazeti ya kiengereza kwa kushirikiana na wahariri na wasanifu wa magazeti ya shirika kabla ya kuchapishwa.
  • Kutekeleza majukumu yote ya kihabari yatakayopangwa na mkuu wako wa kazi katika chumba cha habari pamoja na Mhariri Mtendaji na uongozi wa shirika.
  • Msanifu Gazeti: Nafasi 2 Unguja.

Sifa za muombaji

  • Awe Mzanzibari
  • Asiwe Muajiriwa wa Serikali
  • Awe amemaliza Stashahada ya katika fani ya Teknolojia ya Habari (IT) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uwezo wa kusanifu gazeti na matangazo kwa kutumia program maalumu ya “Adobe Indesign na Photoshop”.
  • Awe na umri usiozidi miaka 40.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta maalum kwa ajili ya kusanifu gazeti na matangazo.
  • Uzoefu wa kazi za usanifu na utayarishaji wa majarida utazingatiwa kama ni sifa ya ziada.

Majukumu ya Kazi:

  1. Kusanifu magazeti ya shirika na kuyaweka katika ubora unaohitajika.
  2. Kupanga kurasa za magazeti katika ubora unaotakiwa kabla ya kuchapishwa.
  3. Kubuni njia mbadala ya kuyapendezesha magazeti ya shirika na kuwa katika kiwango bora.
  4. Kusanifu majarida yanayochapishwa na Shirika
  5. Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
  • Afisa Biashara na Uwekezaji: Nafasi 1 Unguja

Sifa za Mwombaji.

  • Awe Mzanzibari
  • Asiwe Muajiriwa wa Serikali
  • Awe amemaliza Shahada ya Kwanza katika fani ya Uchumi, Biashara au Uwekezaji kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  • Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza kwa ufasaha.
  • Awe na umri usiozidi miaka 40.
  • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
  • Uzoefu wa kazi za biashara ya uchapishaji, uchumi na uwekezaji, itazingatiwa kama sifa ya ziada.

 Majukumu ya Kazi

  • Kusimamia Biashara na Uwekezaji wa Shirika.
  • Kubuni vyanzo vipya ya kukusanya mapato ya Shirika.
  • Kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara na Uwekezaji baina ya Shirika na taasisi nyengine.
  • Kuhakikisha kuwa shirika linaongeza wateja katika ununuzi wa gazeti na bidhaa nyengine pamoja na kuwabakisha waliopo ili malengo ya ukusanyaji mapato yaliyopangwa yafikiwe kwa ufanisi.
  • Kusimamia mkakati wa masoko na uwekezaji ili kuongeza mapato ya Shirika.
  • Kuwezesha upatikanaji wa matangazo mapya kutoka sekta binafsi na sekta za umma
  • Kufanya kazi nyengine zinazolingana na majukumu yake kama atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Utaratibu wa Kuwasilisha Maombi.

Barua za maombi ziandikwe kwa mkono na ziwasilishwe kwa nakala laini (softcopy) kupitia baruapepe barua@smsz.co.tz na nakala ngumu (hardcopy) zitumwe kutumia anuani ifuatayo.

Mhariri Mtendaji,

Shirika la Magazeti ya Serikali,

S.L.P 1893,

Maisara – Zanzibar.

Waombaji wawasilishe maombi yao katika ofisi za SHIRIKA zilizopo Maisara kwa Unguja, Kilimatinde Chake Chake Pemba na Magogoni Dar es Salaam kuanzia tarehe ya 20/09/2024 kuanzia saa 1:30 hadi saa 09:30 alasiri.

Barua za Maombi ziambatanishwe na vielelezo vifuatavyo: –

  • Maelezo binafsi ya muombaji (CV).
  • Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo.
  • Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
  • Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari
  • Picha (1) ya Passport size iliyopigwa karibuni
  • Cheti cha TCU kwa waombaji waliosoma nje ya nchi

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 30/09/2024 Saa 09:30 Alasiri.

Tangazo hili pia linapatikana katika tovuti ya Shirika la Magazeti ya Serikali www.zanzibarleo.co.tz

Pamoja na Mitandao ya Kijamii ya Shirika kama ifuatavyo:-

Instagram: https://www.instagram.com/zanzibarleo_online/

Facebook: https://www.facebook.com/zanzibarleo.online

X (Twitter): https://twitter.com/znzleoonline