Skip to content

Trump, Harris watupiana lawama kwenye mdahalo kampeni za uchaguzi

WASHINGTON, MAREKANI

KAMALA Harris na Donald Trump wamepambana katika mdahalo wa kwanza wa wawili hao ikiwa ni sehemu ya kampeni za uchaguzi wa 2024.

Harris, makamu wa rais wa Marekani na mgombea wa Chama cha Kidemokrasia, na Trump, mteule wa Republican, walikabiliana katika mdahalo huo huku kila mmoja akitaka kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa Novemba 5.

AFP ilikagua usahihi wa kile washindani wote walisema juu ya maswala muhimu ikiwa ni pamoja na uchumi.

Alipoulizwa kama Wamarekani walikuwa na maisha bora kuliko miaka minne iliyopita, Harris hakutoa jibu la moja kwa moja. Alimshutumu Trump kwa “ukosefu mbaya zaidi wa ajira”.

“Huu ni upotoshaji. Ukosefu wa ajira uliongezeka kwa asilimia 14.8 mnamo Aprili 2020 wakati janga la Uviko lilijikita Marekani wakati Trump anaondoka ofisini ukosefu wa ajira ulikuwa asilimia 6.4.

“Tulichofanya ni kusafisha uchafu wa Donald Trump,” Harris ameongeza.

Trump alijibu, akisema maprofesa wa uchumi wameuchukuliwa mpango wake wa kiuchumi kuwa “wa kipekee”, na “mzuri zaidi”.

Katika suala la uhamiaji, Trump ametoa madai yasiyo na msingi kwamba wahamiaji wanakula wanyama katika eneo la Springfield, Ohio.

“Wanakula mbwa. Wanakula wanyama wa nyumbani wa watu wanaoishi huko,” Trump alisema.

Hata hivyo, muongozaji wa mdahalo huo David Muir alibainisha kuwa meneja wa jiji huko Springfield amesema hakuna ushahidi wa dai hilo.