Skip to content

Udaku katika soka

Matheus Cunha
ARSENAL wamefanya mazungumzo ya awali na mshambuliaji wa Wolves raia wa Brazil, Matheus Cunha (25). (Caught Offside).

Virgil van Dijk
BEKI wa Uholanzi, Virgil van Dijk, amepokea ofa ya mkataba kutoka Liverpool, lakini, haiendani na matarajio ya mchezaji huyomwenye umri wa miaka 33. (Athletic).

Julen Lopetegui
MUSTAKABALI wa Julen Lopetegui kama kocha mkuu wa West Ham upo kwenye mizani huku Edin Terzic, Roger Schmidt, Sergio Conceicao na Massimiliano Allegri wakiwa ni miongoni mwa wanaowaniwa kurithi mikoba yake.(Telegraph).

Graham Potter
WEST Ham pia inavutiwa na kocha wa zamani wa Brighton na Chelsea, Graham Potter. (Times).

Rodri
RODRI ameiomba Manchester City kumnunua mchezaji mwenzake wa kimataifa na winga wa Athletic Bilbao, Nico Williams (22). (Metro).

Harry Maguire
BEKI wa England, Harry Maguire (31), anawaniwa klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England huku mushtakabali wake katika Manchester United ukiwa haujulikani. (Football Insider).

Luis Enrique
KOCHA wa Paris St-Germain, Luis Enrique hataki klabu hiyo ya Ufaransa kumleta mshambuliaji wa Sporting na Sweden, Viktor Gyokeres (26), ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester City na Manchester United. (Foot Mercato).

Antoine Semenyo
KLABU ya Newcastle United inawafuatilia winga wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo (24), na mshambuliaji wa Brentford wa Cameroun, Bryan Mbuemo (25). (The i News).

Gabriel Pec
ARSENAL na Liverpool wanamfuatilia winga wa LA Galaxy mwenye umri wa miaka 23 kutoka Brazil, Gabriel Pec. (Caught Offside).

Ruben Selles
KLABU ya Hull City wanatazamia kumteua mkufunzi wa Reading, Ruben Selles kama kocha wao mpya, huku Alex Neil na Slavisa Jokanovic wakiwa miongoni mwa wengine wanaowania nafasi hiyo. (Telegraph).

Daniel Cummings
KLABU za Ligi Kuu zinamfuatilia mshambuliaji wa Celtic mwenye umri wa miaka 18, Daniel Cummings. (Mail).

Rylan Brownlie
KLABU ya Crystal Palace inatazamiwa kumsajili mshambuliaji wa Australia Rylan Brownlie (17) kwa uhamisho wa bure. (Football Insider).