Torshin, ambaye ni mwanachama wa maisha wa NRA, na Butina walihudhuria hafla za NRA huko Marekani kuanzia 2014. Alihudhuria pia hafla ya kampeni ya Trump na inasemekanaalimuuliza Bw Trump maoni yake juu ya uhusiano wa nje na Urusi.
Anna Chapman: Mnamo mwezi Julai mwaka 2010, kulifanyika hafla ya kuwafichua watu 10 waliodaiwa kuwa majasusi wa Urusi kukamatwa na shirika la FBI nchini Marekani, watu hao walikuwa wameishi Marekani kwa muda mrefu sana na hata kuendelea na maisha ya kifamiliakama Wamarekani wengine.
Majasusi wa Marekani walikuwa wamewafuatilia kwa takriban miaka 10 kabla ya kukamatwakwao na baadaye kurejeshwa Urusi.
Miongoni mwa waliokamatwa ni mwanamke mmoja ambaye urembo wake uliviutia vyombo vyahabari kote ulimwenguni huku picha zake zikichapishwa katika majarida mbali mbali na watu wengi wakitaka kujua mengi kumhusu Anna Chapman na wakati huo alikuwa na umri wa miaka28.
Jina lake halisi hata hivyo ni Anna Kushchenko na alikuwa binti wa mwanadiplomasia mmojamkuu wa Urusi aliyesomea Volgograd na Moscow.
Anadaiwa kuishi Uingereza kwa miaka mitano akihudumu katika sekta ya fedha na hata aliolewana raia wa Uingereza Alex Chapman kati ya mwaka wa 2002 na 2005, alibakia kuwa na jina la pili la Chapman hata walipotengana.
Chapman baadaye aliliambia gazeti la Daily Telegraph kwamba hakushangazwa na yaliyomsibumke wake wa zamani, kwani alikuwa amebadilika sana katika ndoa yao na alikuwa akifanyamikutano ya siri na rafiki zake wa Urusi.
Mumewe huyo wa zamani pia alifichua kwamba mke wake wakati wakiwa pamoja alimuelezakwamba babake alikuwa ofisa wa ngazi ya juu wa shirika la ujasusi la zamani la Urusi KGB na kwamba angefanya lolote aliloagizwa na baba yake.
Anna Kushchenko hakuficha uhusiano wake na Urusi alipowasili mjini New York kutoka Moscow mnamo mwezi Februari mwaka wa 2010 akisema alitaka kuanzisha kampuni ya ajirailiyowalenga wanataaluma katika miji yote miwili.
Baadaye Anna Kushchenko alikuwa miongoni mwa maajenti wa Urusi waliokabidhiwa Moscow wakati nchi hizo mbili zilipobadilishana majasusi waliokamatwa katika ngome ya kila mmojawao.
Mengi kumhusu Anna Kushchenko yangali yameghubikwa na usiri mkubwa, lakini wajibu wake na operesheni za ujasusi za Urusi pia bado hazijatoa ufunuzi kuhusu jukumu lake katika sakatahiyo nzima.