NA SAIDA ISSA, DODOMA
BARAZA Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa UVCCM kwa kauli moja limelaani vikali mtu mmoja mmoja vyama vya siasa, asasi za kiraia za ndani na nje ya nchi na jumuiya za kimataifa wanaowatumia vibaya vijana katika kuharibu na kubeza amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi CCM Mohamed Ali Mohamed alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha kawaida cha baraza kuu la umoja wa vijana wa CCM.
“Sisi kama UVCCM tunalaani vikali vitengo viovu vinavyowatumia vijana wetu ama kuwahusisha katika matukio hayo na hatutafumbia macho matukio hayo,”alisema.
Aidha Baraza hilo liliwataka vijana wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kujiandikisha katika daftari la mkazi,kugombea na kupiga kura na kwamba UVCCM itawaunga mkono.
“Baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kwa kauli moja tunazipongeza serikali zetu mbili serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar chini yad kt.hussein ali mwinyi kwa namna zinavyoendelea kuwatumikia wananchi kwa vitendo kupitia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi yam waka 2020-25,”alisema.