Skip to content

Waziri Haroun aeleza mkakati wa  kuimarisha mawasiliano, uchumi

  • Zanzibar

NA MWANAJUMA MMANGA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, KatibaSheria na Utumishi wUmmaHaroun Ali Suleiman, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawathamini wananchi wake ndio maana inaendelea kujenga barabara za kisasa ili kurahisisha mwasiliano na kuimarisha uchumi wao.  

Waziri Haroun aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kidimni –Ubago, wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unmguja, ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar.

Alisema kufunguliwa kwa barabaraba hiyo kwa matumizi ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo kwani kutatanua wigo  na kuimarisha uchumi wa watu wa maeneohayo wakiwemo wakulima, wafanyabiashara na kinamama pale wanaokwendakujifungua.

“Bila shaka wananchi wa maeneo hayo wanajivunia na matunda ya mapinduzikwani kwao ni faraja hivyo ni vyema kuhakikisha tunaendeleza kutunzamiundombinu hiiili itusaidia kwa usafiri wa watu na mazao yanapoyatoamashambani.

“Serikali ya awamu ya nane inayopongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, imetekeleza mambo mengi kwa ajili ya maendeleo makubwa wananchi ambapo zaidi ya asilimia tisa ya miradi imetekelezwa hapa Zanzibar”, alieleza.

Hivyo Waziri huyo aliIshukuru Kampuni ya IRIS kwa hatua nzuri waliojengabarabara hiyo, hivyo aliwataka vijana kuuweka mbele uzalendo na kuipenda nchiyao ili nchi iweze kupiga hatua nzuri ya kimaendeleo.

Sambamba na hilo aliwaomba viongozi wa mkoa huo kuhakikisha wanakuwa na mashirikiano ya karibu wananchi wao katika kuhakikisha kusaidia kufikia malengoya chama   cha Mapinduzi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na UchukuziZanzibar, Machano Makame Haji, akitoa taarifa ya kitaalamu, alisema barabrab ya Kidimni – Ubago inaurefu wa kilo mita 4.3, ambapo inaunganisha na barabrabamikoa Kusini na Kaskazini pamoja na mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha alisema barabra hiyo ni miongoni mwa barabara zilizopangwa kujengwakwenye wilaya ya kati ikiwa ni sehemu ya kuunganishwa mikoa ya Unguja na kuongeza kuwa barabara hizo zenye urefu wa kimomita 275 zikigharimu Dola80,300,000  za Marekani.

“Ujenzi wa barabara hii ulianza Novemba 11, 2022 na kujengwa kwa kiwango cha lami  aina ya chipsi  hivyo srikali iliona umuhimu wa kuiongezea uwezo kwa lengola kuzifanya iweze kutumika kwa magari ya aina zote na wakati wote”, alieleza.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud, alisema mkoa huo una miradi isiyopungua 16 ambayo ni jitihada ya serikali za kuondosha changamoto kwa wananchi wa mkoa huo.

Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huo kuitunza na kuithamini jitihada za serikali hiyo ambayo inayoongiozwa na Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kuungamkono jitiohada za wananchi wake ili kuona wanaondokana na changamoto ya huduma za barabara.

Ayoub alisema kuna baadhi ya viongozi wamekuwa wakigawa makundi wanachiwao hivyo aliwataka viongozi hao kuacha tabia ya uchonganishi ili kuiweka nchikatika hali ya usalama na amani.

Alisema ujenzi wa bararaba hiyo ni maendeleo makubwa  kwani mkoa huoumebarikiwa na barabara za lami wa zaidi ya asilimia 70 sambamba na kuwa na daraja la Uzi ambalo litawafungua wananchi wa Uzi kimaendeleo na Kusini kwa Ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mbunge wa jimbo la Uzini, Khamis HamzaChilo, alisema ufunguzi wa jimbo hilo ambalo limeunganisha majimbo mawiliUzini, Kiboje alimshukuru Rais kwa hatua ya kuwajengea barabrab hiyo ambapohapo awali ilikuwa ni malalamiko na kero kwa wananchi lakini itakwendakutumika kwa wananchi kwa shughuli mbali mbali za kijamii, uchumi na kiutamaduni.