Skip to content

WEMA, ZICTIA zasaini mkataba kuunganisha skuli 100 Mkongo wa Taifa 

  • Zanzibar

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali, imetiliana saini hati za mashirikiano na Shirika la Mawasiliano la Zanzibar (ZICTIA) kwa ajili ya kuweka Mkonga wa mawasiliano kwa skuli 100 za Unguja na Pemba.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Mohamed Mussa alisema mradi huo umelenga kuhakikisha elimu inakuwa kidijitali zaidi.

Waziri huyo alisema lengo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ni kuleta mageuzi katika sekta ya elimu ambapo miongoni mwa maeneoyenye vipaumbele ni katika TEHAMA ikiwemo kuboresha miundombinu katika skuli za Zanzibar.

Lela alimpongeza Dk. Mwinyi kwa kuruhusu kutumika kiasi cha dola milioni tatu kwa ajili ya elimu na kuwataka wizara, ZICTIA na Dolfin kutimiza lengo la Rais la kuleta mageuzi makubwakatika sekta hiyo liweze kufikiwa.

Aidha alisema kuwepo kwa miundombinu hiyo kutasaisia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhabawa walimu wa sayansi na walimu watatoka kufundisha kwa kutumia chaki.

Hivyo, aliwataka walimu waliokuwepo katika vituo vya kisayansi, TEHAMA na skuli kubadilika na kuhakikisha wanasimamia walimu kutumia miundombimu hiyo kwa ajili ya kutayarisha masomo na kufundishia wanafunzi na kuwa wabunifu.

Aliipongeza Benki ya Dunia kwa mashirikiano waliyoyatoa na kuahidi kwamba wataifanyia kazikama walivyokusudia katika mipango ya awali katika sekta ya elimu. 

Sambamba na hayo alisema ni matumaini yake kuwa ZICTIA itafanya kazi hiyo kwa mudawaliokubaliana katika mkataba kwa kuhakikisha skuli zote zimeunganishwa na mkonga wa mawasiliano na kampuni ya Dolfin italeta vifaa ambavyo vina ubora waliokubaliana.    

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Khamis Abdalla Said, alisema mkataba huo, unalengakuziunganisha baadhi ya skuli na mkonga wa taifa kwa masharti ya kuwa na ‘O data’.

Alisema vituo hivyo vitakuwa vinapokea maudhui ya elimu ambayo wizara inatayarisha na kuhifadhi katika ‘saver’ na skuli itapata maudhui bila ya kutumia fedha kwa ajili ya mtandao.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, HawwahIbrahim Mbaye, aliipomgeza wizara kwa hatua hiyo kwani wanafarajika kuona Tehama sasainakwenda kufika kwa jamii ambapo ndio lengo la serikali.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA), Shukuru Awadhi Suleiman, aliipongeza WEMA kwa imani yao ya kushirikiana kuunganisha skuli za Zanzibar na mkonga wa taifa wa mawasiliano ili wanaafunzi waweze kusoma kwa kutumia tehama.

Aliahidi kuwa mradi huo utafanyika kwa muda uliopangwa kama walivyoahidi katika makubaliano yao kwa kipindi cha wiki 24 na kuiomba wizara kuharakisha kusaini mashirikianokwa awamu ya pili.

Alisisitiza utunzaji wa vifaa wanavyoviweka katika skuli na kutoa elimu ili kuona fursa hiyo inawafikia walimu na wanafunzi wote kwa ujumla kuona wanatumia miundombinu hiyo.

Mbali na hayo, alisema ili kwenda sambamba na mapinduzi ya teknologia Rais Mwinyiametoa eneo lenye hekta 71 kwa shirika hilo kwa ajili ya kujenga mji wa tehama katika eneo la Fumba.

Mapema Mkurugenzi wa Tehama Zanzibar kutoka WEMA, Mbwana Yahya Mwinyi, alisema mashirikino hayo yamelenga kuziunganisha skuli zote za Zanzibar na Mkonga wa mawasiliano ikiwemo vituo vya ubunifu wa kisayansi 11 na vituo vya Tehama 20 na skuli zote za serikali ikiwemo skuli 26 mpya za msingi na sekondari ili kuona skuli zote ziwe na mkonga.