Skip to content

Silaa aanza ziara ya kikazi Kilimanjaro

  • Bara

NA SAIDA ISSA

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry William Silaa,  amewasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, ambapo amepokelewa rasmi na mwenyeji wake, Nurdin Babu, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Ziara ya Silaa inalenga kukagua na kutathmini hali ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika mkoa huo, hususani eneo la Mkomazi.

Silaa amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora na ya uhakika ya mawasiliano, bila kujali eneo analoishi.

Katika salamu zake za awali, Babu alimkaribisha waziri Silaa na kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika kuhakikisha miundombinu ya mawasiliano inaongezwa na kuboreshwa nchini kote.

Silaa anatarajiwa kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro ili kujionea changamoto na mafanikio katika sekta ya mawasiliano, ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi kwa lengo la kupata mrejesho wa moja kwa moja kutoka kwa walengwa wanaotumia huduma za Mawasiliano.