Skip to content

Israel yataka kuweka kituo cha kijeshi Somalia

MOGADISHU, SOMALIA

Utawala Israel unataka kuwa na kituo cha kijeshi kaskazini mwa Somalia, kupitia eneo lililojitangazia uhuru wake la Somaliland.

Endapo Somaliland ambayo imetangaza kujiondoa kwenye taifa la Somalia itakubali kuruhusu bila ya idhini ya Somalia kunaweza kukaibuka mvutano.

Kwa mujibu wa Middle East Eye, utawala wa Israel unakodolea macho ya tamaa eneo la kaskazini mwa Somalia kwa shabaha ya kuwa na kituo cha kijeshi kitakachokuwa kinaangalia kwa karibu safari za baharini za lango bahari la Bab al Mandab la nchini Yemen.

Katika mkabala wa suala hilo, utawala wa Israel unapanga kuitambua rasmi Somaliland kuwa ni nchi licha ya sheria zote za kimataifa kuonesha kuwa hilo ni eneo ambalo haliwezi kutenganishwa na maeneo mengine ya Somalia.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa njama za kuweka mikataba na kujaribu kutambua uhuru wa Somaliland zinahatarisha usalama wa nchi za eneo hilo.

Somalia inapinga kutambuliwa kwa Somaliland kwa kile inachokieleza kuwa ni sehemu ya nchi yake.