Skip to content

Udaku katika soka

RANDAL KOLO

MANCHESTER UNITED wana nia ya kumsajili mshambuliajiwa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, kutoka PSG na huenda likawa chaguo la mkopo ambalo lina kifungu cha kumnunua kabisa mwezi Januari. (L’Equipe- Ufaransa).

ANDREAS CHRISTENSEN

NEWCASTLE UNITED wanalenga kumnunua mlinzi wa Barcelona Andreas Christensen, 28, na kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark kunaweza kuruhusu klabu hiyo ya La Liga kumsajili mshambuliaji wa Hispania Dani Olmo, 26. (Fichajes – in Spanish),

KIERAN TRIPPIER

NEWCASTLE wanapanga kumuuza beki wa kushoto wa Uingereza Kieran Trippier, 34, na kiungo mshambuliaji wa Paraguay Miguel Almiron, 30, ili kusaidia msimamo wao linapokuja suala la sheria za faida na uendelevu. (Football Insider),

CARNEY CHUKWUEMEKA

CHELSEA wako tayari kuwaruhusu wachezaji wa kati wa Uingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 26, na Carney Chukwuemeka, 21, kuondoka kwa mkopo katika klabu hiyo mwezi Januari. (Mirror)

DEWSBURY-HALL,

LEICESTER CITY wanapanga kumrejesha klabuni Dewsbury-Hall, baada ya kumuuza kwa Chelsea katika majira ya joto. (Football Insider)

GRAHAM POTTER

MENEJA wa zamani wa Brighton na Chelsea Graham Potter alikataa nia ya Wolves mwezi uliopita huku klabu hiyo ya Midlands ikitafuta chaguo kuchukua nafasi ya Gary O’Neil, ambaye kwa sasa ametimuliwa. (Guardian)

NICOLAS JACKSON

MSHAMBULIZI wa Senegal Nicolas Jackson nusura ajiunge na Aston Villa na Bournemouth kutoka Villarreal Januari 2023 kabla ya kwenda Chelsea. ( 90min)

CHRISTIAN PULISIC

KLABU ya AC Milan ya Italia inakaribia kumpata mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic mwenye umri wa miaka 26 kwa mkataba mpya. (Fabrizio Romano)

TIJJANI REIJNDERS

AC MILAN pia wanatazamia kuongeza mkataba wa kiungo wa kati wa Uholanzi Tijjani Reijnders na kipa wa Ufaransa Mike Maignan kwa masharti mapya na yaliyoboreshwa. (Calciomercato – In Itali)