Skip to content

Dk. Mwinyi anogesha furaha Zanzibar Heroes 

NA KHAMISUU ABDALLAH 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi anatarajia kuunda kamati maalum ya kumshauri namba bora ya kukuza soka la Zanzibar. 

Dk. Mwinyi alieleza hayo katika hafla ya chalula cha mchana aliyoiandaa kwa ajili yakuwapongeza mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Cup timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

Alisema kamati hiyo pamoja na mambo mengine, kamati hiyo italazima kupendekeza namnasoka la Zanzibar litakavyoimarishwa.

Aidha alisema kamati hiyo itakuwa na wabobezi katika masuala ya michezo ili waweze kumpaushauri mzuri lakini pia na madhumuni ya kuwa na timu imara zaidi kutoka chini mpaka katika taifa. 

Dk. Mwinyi akizungumzia ushindi uliopatikana katika fainali ya mashindano ya Mapinduzi Cup kwa timu ya Zanzibar Heroes kupata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya timu Burkina Faso alisema inaonekana Zanzibar ina kiwango kikubwa cha mpira wa miguu kutokana na ushindiunaopatikana.

Dk. Mwinyi alibainisha kuwa hatua hiyo inamaanisha kwamba Zanzibar ina vipaji na kwambakinachohitajika ni kuwezeshwa vijana ili waweze kufanya vizuri zaidi.

Alisema katika kuwawezesha vijana serikali ina mpango wa kujenga akademi ya soka kila mkoaili kuibua zaidi vipaji.

“Nimepokea simu kutoka Uturuki wakanambia tulikuwa tunatizama mechi, naona mna vijana wanatufaa vipi tuje nikawaambia njoni. Wameniahidi watakuja kuwachukua vijana wenye vipajikwenda kufanya majaribio ya soka”, alisema.

Dk. Mwinyi aliipongeza Zanzibar Heroes kwa kazi nzuri waliyoifanya katika mashindano hayo na kuiletea ushindi Zanzibar, ambapo wameipatia heshima nchi kwa kulibakisha nyumbanikombe la Mapinduzi 

Hata hivyo, Dk. Mwinyi alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdullah kwa kusimamia sherehe za Mapinduzi kwa ujumla ikiwemo kufanikisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Aliipongeza Wizara kwa kazi nzuri waliyoifanya na wadhamini wa mashindano hayo na kuwaomba kuendelea kudhamini kwani mashindano hayo yanafanyika kila mwaka. 

Naye Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Maulid Mwita, alimpongezaMakamu Hemed kwa kufanikisha mashindano hayo.

Alisema mwaka huu walipata changamoto kubwa wadhamini wengi walikuwa wanabana kamawanapoekeza fedha yao Pemba kama itakuwa hairudi kwa mujibu wa taratibu zao.

“Tulikuwa tuna kazi kubwa ya kuelimisha lakini mpaka dakika za mwisho wadhaminihawakutoa na walituahidi ili jambo kwa kweli limedhorotesha baadhi ya mambo katika Kombela Mapinduzi,” alisema. 

Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Suleiman Mahmoud Jabir alimpongeza Rais Mwinyi kwa kuwathamini na kusherehekea ushindi kwa timu yao wakiwamabingwa kwa mwaka 2025 kwa kombe la Mapinduzi.

“Tumeionesha dunia kama Zanzibar tuna vipaji na kama tutapata fursa na kupata nafasi katika mashindano ya kimataifa naamini kabisa tunaweza kufanya makubwa na mazito zaidi,” alisema.

Aliwapongeza wadhamini wahisani na wadau wote na anaamini dhamira ya Dk. Mwinyi itatimiakatika michezo na anayoyataka kuyaona basi wataendelea kumpa raha kupitia michezo.

Hemed Suleiman Moroko ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes, alisemaZanzibar ina vipaji vikubwa na anaamini itafika mbali katika sekta ya michezo.

Alimkabidhi Rais Mwinyi timu hiyo na kumuomba kuwanulia vifaa vya kisasa ikiwemo kifaacha kipima masafa (GPS).

Katika halfa hiyo Rais Mwinyi alikabidhi zawadi kwa timu hiyo shilingi milioni 50,000,000 na wadau wengine waliotoa zawadi hiyo ni Baraza la Wawakilishi shilingi 10,000,000, PBZ shilingi10,000,000, CRDB 15,000,000 na Rahisi Solution 10,000,000.