RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujenga uwanja mkubwawa michezo wenye hadhi ya kimataifa, kitakachotumika kwa michuano ya kimataifaikiwemo michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027.
Dk. Mwinyi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na wadau wa michezo waliohudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa viwanja vya michezoMaisara (Maisara Sports Complex), mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni muendelezo wa shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“Tuna dhamira ya kweli ya kujenga uwanja wa kisasa wa AFCON utakaofanana na ule wa ‘Old Traford’ wa Manchester United ya Uingereza” Alisisitiza Rais Dk. Mwinyi.
Alieeleza kuwa Zanzibar ikiwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja nchi za Kenya na Uganda watakuwa wenyeji wa michuano ya AFCON mwaka 2027 hivyo hatua hiyoinakwenda sambamba na kufanyiwa marekebisho makubwa ya viwanja vya Gombani Pemba na uwanja wa Mao Zedong ili kupata viwanja vya kisasa vitakavyokuwa chachu ya kuwainua vijanakimichezo.
“Dhamira nyengine ya serikali ni kujenga kiwanja cha mpira wa ufukweni (Beach soccer) kwa hadhi ya kimataifa na kujenga bwawa kubwa la kuogelea (Swimming pool) lenye hadhi ya Olympic, (Olympic size Swimming pool)”, aliongeza Dk. Mwinyi.
Alieleza hali hiyo imepitwa na wakati, hivyo serikali imejiandaa kujenga viwanja vipya ili kutoafursa kwa vijana kuinua vipaji vyao na ushindana kimataifa na kueleza kuwa bado Zanzibar inatamani kurudi kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) hivyo ujenziwa viwanja hivyo ni chachu itakayoleta ushawishi wa kupata uanachama huo.
Aidha Dk. Mwinyi alifahamisha kuwa kuna kila sababu ya Zanzibar kuwa mwanachama waCAF kwa sababu ina timu mahiri ya taifa (Zanzibar Herros) inayoweza kuleta ushindani na vikombe vingi nchini.
Akizungumzia viwanja vya Maisra Sports Complex, Dk. Mwinyi, aliwashukuru viongozi waWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kwa kusimamia kikamilifu maendeleo ya ujenzi huo ambao kwa kiasi kikubwa utaimarisha sekta ya michezo nchini.
Alieleza kuwa viwanja hivyo vitajumuisha viwanja vya michezo mbali mbali ukiwemo mpira wakikapu (basketi ball), mpira wa wavu (volleyball), mpira wa mikono (hand ball) na mchezo wa tenis utakaotoa mazingira bora kwa vijana kujifundisha michezo hiyo na kuzalisha vipaji zaidi.
“Nimefurahishwa na kuwepo kwa kituo cha mazoezi ya viungo katika viwanja hivi pamoja na viwanja vya kufurahishia watoto (Children playground) jambo litakalotoa nafasi kwa watotowetu na vijana kukuza vipaji vyao”, alieleza.
Akizungumzia kaulimbiu ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar isemayo ‘Amani, Umoja naMshikamano kwa Maendeleo yetu’ aliwasihi wananchi kutokubali kufitinishwa ili maendeleozaidi yaendelee kupatikana katika sekta mbalimbali.
“Bila ya Amani, Umoja na Mshikamano hakuna suala lolote la maendeleo litakalofaikiwa” alibainisha Rais Dk. Mwinyi.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TabiaMaulid Mwita, alisema wizara itaendelea kutekeleza na kufuata maelekezo na miongozoinayotolewa na Dk. Mwinyi kwa kukamilisha miradi yote inayosimamiwa na Wizara hiyo kwa wakati na mafanikio.
Waziri Tabia alieleza kuwa kinachofanyika hivi sasa katika viwanja vya michezo Unguja na Pemba ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, 2020 -2025 kwa vitendo na kumuhakikishiaRais kuwa viwanja hivyo vitatunzwa na kulindwa kwa viwanja vyote vinavyojengwa ili vitumikekwa miaka mingi iyajo.
Akiwasilisha taarifa ya kitaalamu kuhusu mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, FatmaHamad Rajab, alisema ujenzi wa viwanja vipya vya ‘Maisara Spots Complex’ ulianza Septemba2024 na unatarajiwa kukamilika Machi 2025 ambapo kwasasa umefikia 60 % ya ujenzi wake na mkandarasi anaendeleza ujenzi huo kwa kasi inayoridhisha.
Aliongeza kuwa ujenzi wa viwanja vipya vya michezo vya Maisara ni miongoni mwa ujenzi wa viwanja 17 vya michezo Unguja na Pemba vyenye viwango vinavyokubalika na CAF na FIFA.