Skip to content

Macron auona upande wa pili wa shilingi barani Afrika

  • Makala

WAKATI Ufaransa ikiendelea kupoteza kambi zake kadhaa za kijeshi barani Afrikaraiswa nchi hiyo, Emmanuel Macron, katika safari ya kimyakimya kwenye kituo cha mwishocha operesheni za nchi hiyo huko Djibouti, amekiri kwamba Afrika inapitia kwenyemabadiliko.

Kwa mujibu wa rais huyo sababu kuwepo kwa mabadiko aliyoyashuhidia barani Afrika ni kutokana na maoni ya umma na serikali za nchi hizo na kueleza kuwa nafasi ya Ufaransa banihumo nayo lazima ibadilike.

Katika safari hiyo, Macron amekiri kwamba kambi ya kijeshi ya Ufaransa nchini Djibouti inaweza kuwa na nafasi muhimu zaidi na kukiri kuwa Ufaransa inalazimika kubadilishamtazamo wake wa zamani dhidi ya uwepo wa majeshi yake barani Afrika.

Macron pia ametangaza kuwa majukumu ya kambi ya kijeshi ya Ufaransa huko Djibouti yataangaliwa upya na kusema kambi hiyo inapaswa kutumika kama sehemu ya utumiaji nguvukatika baadhi ya misheni za Ufaransa barani Afrika.

Safari ya Macron nchini Djibouti imefanyika baada ya Ufaransa kupoteza kambi zake nyingi za kijeshi katika nchi tofauti za Afrika, hasa katika eneo la Sahel na Afrika Magharibi. 

Nchi mbalimbali za Afrika kama vile Mali, Burkina Faso, Niger na hivi karibuni Chad ni miongoni mwa nchi ambazo zimefunga kambi za kijeshi za Ufaransa na kuyafukuza majeshi ya nchi hiyo katika ardhi zao. 

Kufukuzwa vikosi vya majeshi ya Ufaransa katika nchi tofauti za Kiafrika kunafanyika licha ya kwamba nchi mbalimbali za bara hilo zilikuwa chini ya udhibiti wa Ufaransa kwa miaka mingi. 

Bila shaka jinai zilizofanywa na Ufaransa wakati ilipoikalia kwa mabavu ya ukoloni nchini Algeria na kisha kuwaua Waalgeria na kuhusika nchi hiyo katika mauaji ya kimbari ya Rwanda na Cameroon ni mambo ambayo kamwe hayawezi kufutika katika kumbukumbu ya kihistoria ya watu wa bara la Afrika.

Licha ya ukweli kwamba Paris ililazimishwa kutambua uhuru wa nchi makoloni yake ya zamanikama vile Algeria katika miongo kadhaa iliyopita kutokana na muamko wa mapambano ya mataifa ya Kiafrika, lakini kamwe haikuondoka kikamilifu barani Afrika. 

Paris imekuwapo katika nchi nyingi za bara hilo katika fremu ya ukoloni mamboleo ikitumiavisingizio mbalimbali kama vile kurejesha usalama, kupambana na ugaidi na kusaidia kuboreshahali ya kiuchumi.

Bara la Afrika lina umuhimu maalumu kwa Ufaransa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijeshi.

Kwa mfano, katika nyanja za kiuchumi, hadi 2020, makampuni ya Kifaransa yalikuwa yakihodhikaribu uzalishaji wa rasilimali za madini katika makoloni ya zamani ya nchi hiyo kama Niger na Mali.

Aidha kwa sehemu kubwa ya mahitaji ya madini ya uranium yanayotumiwa na Ufaransa kwa ajili ya nishati katika vinu vya nyuklia vya Ufaransa ilikuwa ikitolewa katika nchi ya Niger.

Katika sekta ya masuala ya kijeshi, vikosi vya Ufaransa vimekuwepo katika nchi tofauti za Kiafrika na mara nyingi vimekuwa vikisimamia kamandi za kijeshi. 

Katika muktadha huu, tunaweza kutaja uwepo wa jeshi la Ufaransa katika nchi kama Mali, Niger, Ivory Coast na Chad kwa kisingizio cha kusaidia kuimarisha usalama na amani na kupambana na ugaidi katika miaka 10 iliyopita, na Ufaransa ilikuwa na kambi rasmi za kijeshikatika baadhi ya nchi hizo.

Ingawa katika miaka 10 iliyopita, Ufaransa katika mfumo wa ukoloni mamboleo, ambaoulijaribu kuibakisha nchi hiyo barani Afrika kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia visingiziokadhaa.

Visingizio hivyo ni pamoja na kuchangia misaada ya kifedha, kutekeleza miradi ya kiuchumi na kibiashara, kutoa mikopo, kujenga viwanda na vituo vya kijeshi, lakini hulka ya kikoloni na uhalifu wa nchi hiyo havikusahauliwa na umma wa Waafrika, kiasi kwamba katika miakamichache iliyopita, nchi nyingi za Kiafrika zilitaka rasmi kukomesha uwepo wa kijeshi wa Ufaransa katika bara lao na kufukuzwa vikosi vya kijeshi vya nchi hiyo. 

Katika nchi za Mali, Burkina Faso, Niger, na Chad ni miongoni mwa nchi ambazo zimeyatimuarasmi majeshi ya Ufaransa na kuchukua udhibiti wa mambo yao wenyewe. 

Suala hili limewachukiza sana viongozi wa Ufaransa na hata nchi nyingine za kikoloni za Ulaya. Pamoja na hayo wakoloni hao wa zamani wanapasa kukubali hali halisi ya mabadiliko ya duniayalivyo kwa wakati huu.

Ni kwa msingi huo ndiyo maana Catherine Colonna, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ufaransa, amekiri rasmi kwamba enzi ya ukoloni wa nchi hiyo barani Afrika zimekwisha na kwamba kinachoshuhudiwa ni kushamiri kwa wimbi la chuki dhidi ya Ufaransa barani Afrikahumo.

Pamoja na hayo Wafaransa na wakoloni wengine wanapaswa kutambua kuwa Waafrikahawawachukii Wafaransa kama Wafaransa, bali wanachukia ukoloni, ubabe, kuporwa mali na rasimali zao.

Waafria pia wanachukia kudharauliwa, kuonekana watu duni wasio na lolote, kutazamwa kamawatu wa daraja la pili na pengine la tatu na nne na wanachukia wakoloni kujitukuza na kujinufaisha kwa rasilimali zao.