LAMINE YAMAL,
WINGA wa Hispania Lamine Yamal, 17, anakaribia kuongeza mkataba wake na Barcelona hadi 2030. (Nicolo Schira).
JOAO PEDRO
MPANGO wa Liverpool kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Brazil Joao Pedro huenda ukalazimika kusubiri hadi msimu wa joto kwani matakwa ya Seagulls kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yatafanya uhamisho wa Januari kuwa mgumu. (Football Insider),
ALEXANDER ISAK
PARIS ST-GERMAIN wako tayari kulipa euro milioni 100 (pauni milioni83) kumsajili mshambuliaji wa Newcastle United raia wa Uswisi Alexander Isak, 25. (Fichajes.net – in Spanish).
NICO WILLIAMS
PSG ya Ufaransa pia inatazamia kulipa euro milioni 58 (pauni milioni 48) kama kifungu cha kutolewa cha Athletic Bilbao kwa winga wa Hispania Nico Williams, lakini Manchester United na Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (El Desmarque – In Spanish)
FRENKIE DE JONG
BARCELONA wamepoteza imani na kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong na inaonekana kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kuondoka katika klabu hiyo ya Hispania. (Relevo – In Spnish)
VALENTIN GOMEZ
LEICESTER CITY wanapanga mpango wa pauni milioni 8 kumnunua kiungo wa kati wa Argentina Valentin Gomez, 21, kutoka Velez Sarsfield. (Sun)
ERIC GARCIA
NEWCASTLE ni moja ya klabu zinazomtaka beki wa Barcelona Eric Garcia, 23, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City anataka kusalia Nou Camp na kupigania nafasi katika kikosi cha kwanza. (Sport – In Spanish)
JAN-NIKLAS BESTE
CRYSTAL PALACE wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Benfica Mjerumani Jan-Niklas Beste, 25, mwezi Januari. (Sky Sports Switzerland)
RAFA MARIN,
REAL MADRID wanamfikiria beki wa kati wa Hispania chini ya umri wa miaka 21 Rafa Marin, 22, ambaye alifanya mazoezi katika akademi yao ya vijana na kwa sasa anachezea Napoli. (Fichajes.net – in Spanish)
OLI MCBURNIE,
BLACKBURN ROVERS na Burnley wanataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Sheffield United kutoka Scotland Oli McBurnie, 28, kutoka Las Palmas ya Hispania. (Sun),