MWAJUMA JUMA NA ASYA HASSAN
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imesema wakati umefika sasa kuja na mfumo wa kielektroniki wa upimaji utendaji kazi, ili kuongeza ufanisi katika taasisi zao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman alisema hayo alipokuwa akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe Dk, Mohamed Ali Suleima, katika Kikao kinachoendelea cha Baraza la Wawakilishi.
Mwakilishi huyo alitaka kujua kwamba serikali haioni kama sasa muda muafaka wa kuja na mfumo wa kielektoniki wa utendaji kazi, ili kuongeza ufanisi katika taasisi za umma.
Alisema serikali inatumia fomu hiyo kwa ajili ya kuwapimia watumishi wa taasisi za umma Zanzibar, ambapo utekelezaji wake ulianza tangu mwezi Novemba mwaka 2019.
Waziri huyo, alisema Wizara inaimarisha fomu hiyo kwa kuitoa katika mfumo wa menual na kuwa katika mfumo wa kidigitali ili iunganishwe na biometric za mahuzurio na kutoa matukio halisi.
Aidha alifahamisha kuwa katika mfumo uliyopo hivi sasa maksi hutolewa na kiongozi husika kwa namna anavohisi yeye zaidi.