Skip to content

Ruto aahidi kuongeza uwekezaji ili  kuboresha usalama wa baharini

  • Afrika

NAIROBI, KENYA

Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake itaongeza uwekezaji katika sekta ya mambo ya baharini kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na matishio ya mpakani.

Rais Ruto alisema hayo katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Majini la Kenya yaliyofanyika mjini Mombasa, na kuongeza kuwa, serikali itaboresha uungaji mkono kwa jeshihilo ili kuboresha uwezo wake wa kulinda mipaka ya baharini ya nchi hiyo.

Pia amesema, Kenya itaongeza uwekezaji katika teknolojia za juu na kuboresha jeshi la majini, na kwamba serikali pia itaongeza ujuzi na uwezo wa operesheni kwa askari wa jeshi hilo.

Pia amepongeza masikilizano kati ya jeshi hilo na Kikosi cha Ulinzi wa Pwani, na kusema taasisihizo mbili zinalinda maeneo ya pwani ya nchi hiyo, kukabiliana na vitendo haramu, kulindarasilimali za baharini na kulinda njjia za baharini za mawasiliano na biashara.