PEMBA
NYUMBA ya ghorofa moja inayomilikiwa na Shirika la Nyumba kisiwani Pemba, imeteketea kwa moto majira ya saa 2:15 asubuhi katika mtaa wa Bomani shehia ya Selemu Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Wakizungumza na wananchi walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa, watu waliokuwemo waliwahi kutoka ingawa vitu vyao vyote vimeteketea kwa moto.
Walieleza kuwa, baada baada ya kuonekana nyumba hiyo inaungua inaungua ndipo walipowapigia simu wakaazi wa humo, ambapo walifanikiwa kutoka bila kuhamisha kitu chochote.
“Watu waliokuwemo waliwahi kutoka ingawa kuna mwanamke mmoja baada tu ya kufika chini alizimia,” alisema mmoja wa wananchi.
Mwananchi mwengine alieleza kuwa, anahisi tukio hilo limesabasababishwa na hitilafu ya umeme baada ya nyaya kugusana wakati ulipopiga upepo.
Lakini Kikosi chetu cha Zimamoto na Uokozi wamejitahidi sana kuUzima moto huo wakishirikiana na sisi wananchi, ambapo baadhi ya vitu vilivyokuwemo viliokolewa.
Akithibitisha kutokea kwa tokeo hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi William Timoto Mpangale alisema, chanzo cha moto bado hakijajulikana na wala hakuna mtu aliepoteza maisha.