MATAIFA mbalimbali ulimwenguni yanatumia mbinu kadhaa za kijasusi katika kuhakikisha yanadhibiti viasharia vya uvunjifu wa amani na kuimarika kwa usalama wa mataifa hayo.
Katika mataifa kadhaa wanawake kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakitumiwa kwenye shughuliza kijasusi na kiukweli wamekuwa na mafanikio mazuri katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Urusi katika kuhakikisha linapata taarifa za kijasusi kutoka kwa hasimu wake taifa la Marekani, liliandaa wanawake warembo wenye kuvutia na kuwatumia kwa ajili ya kazi ya kijasusi.
Tabasamu za warembo hao zilikuwa za kuvutia, urembo wao ulikuwa kama chambo na mishenizao katika kuhakikisha wanafanikiwa katika majukumu yao zilikuwa za siri kubwa.
Warembo wao walijenga mahusiano ya karibu na wanaume mbali mbali nchini Marekani, ambapo lengo ni moja tu nalo ni kukusanya habari muhimu kuhusu mipango ya siri na mikubwaya serikali ya Marekani na kuhakikisha kwamba Urusi ilifahamu yote yaliokuwa yakiendeleanchini humo.
Wengi waliishi nchini Marekani kwa miaka na hata kuolewa na kuanzisha familia nchini humo. Katika usiri wa maisha yao uliojaa mengi ambayo yalikuwa ni kwa manufaa kwa Moscow.
Baadhi ya warembo waliopewa mafunzo ya kijasusi kuisaidia Urusi kufahamu yote yaliyokuwayakifanyika ndani na nje ya serikali ya Marekani na washirika wake.
Kwa miaka mingi ilishukiwa kwamba Urusi haikuwa imekomesha oparesheni zake za kijasusikatika kiuchunguza Marekani na washirika wake mbalimbali duniani.
Tangu wakati za vita baridi na mapambano ya nchi za magharibi dhidi ya ukomunisti, Urusiiliendelea na oparesheni za siri za ujasusi ambazo mashirika mengine ya ujasusi hasa ya Marekani hayakudhani zingeweza kufanikishwa kwa muda mrefu.
Baadhi ya oparesheni hizo zilihusisha majasusi maalum wa kike ambao walipewa mafunzo na Moscow na kisha kutumwa katika miji ya Marekani ili kukita kabisa ndani ya maisha ya kijamiiya wamarekani na kufichua siri nyingi.